Skip to main content

Posts

ABG NORTH MARA YAGAWA MADAWATI 1,000 KWA SHULE ZA TARIME.

  Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi zilizopo wilayani Tarime mkoa wa Mara wakifurahia msaada wa madawati zaidi ya 1,000 kutoka mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG). Wanafunzi wa shule za msingi za serikali za wilaya ya Tarime, mkoa wa Mara, wakikaa sakafuni kabla ya kupata msaada wa madawati zaidi ya elfu moja kutoka mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG). Msaada wa pikipiki tatu maarufu kama Bajaj ambazo mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) ulitoa kwa baadhi ya wananchi wa jamii zinazoishi karibu na mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara. TARIME Mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) umetoa msaada wa madawati zaidi ya 1,000 kwa shule za msingi zilizopo wilayani Tarime, mkoa wa Mara. Msaada huo utakaoen...

MRADI WA " ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI" WAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

Mwalimu  wa  Ujasiriamali  kutoka  katika  Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation, Mama  Ashankira  Lupembe  , akifundisha  kwa  vitendo  namna  ya  kutengeneza  sabuni   ya  maji. Mwanafunzi  wa  ujasiriamali  akitengeneza  sabuni  ya  unga  mwenyewe  mara  baada  ya  kupata  maelekezo  kutoka  kwa   waalimu  wa  ujasiriamali  kutoka  RafikiELIMU  Foundation. Mwanafunzi  wa  ujasiriamali  akitengeneza  sabuni  ya  maji  kwa  vitendo   mara  baada  ya  kupata  maelekezo  kutoka  kwa   waalimu  wa  Ujasiriamali  kutoka  katika  Asasi  ya  RafikiElimu  Foundation. Wajasiriamali  wakifanya  "  practical "  ya  kutengeneza ...

ORODHA YA MAJINA YA WAJASIRIAMALI WA JIJINI DAR ES SALAAM WALIO JIANDIKISHA KATIKA MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI.

Yafuatayo  ni  majina   ya   vijana  wa  kitanzania  walio  jiandikisha  katika  awamu  ya  kwanza  ya   Mradi  wa  Elimu  ya Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini  "   EUMIVI   PROJECT . mbao  utaanza  rasmi  siku  ya  jumamosi  ya  tarehe  01  Septemba  2012   kuanzia  saa  nne  kamili  asubuhi  katika  Shule Ya  Msingi  Mlimani  iliyopo  katika  eneo  la  Chuo  Kikuu  Cha  Dar  Es  salaam.  Kwa  jijini  Dar  Es  salaam, mafunzo  yatachukua  siku  tatu, kuanzia  tarehe  01 Septemba  2012  hadi  tarehe 03 Septemba  2012. Baada  ya  hapo mradi  utaendelea  katika  miji  ya Arusha, Morogoro, Mwanza, Mbeya, Dodoma...

TAARIFA KUHUSU UZINDUZI WA MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI.

  Uongozi  wa   RafikiElimu  Foundation,   unapenda   kuwa  julisha    wajasiriamali  wote  walio  jiandikisha  katika   Mradi  Wa  Mafunzo  Ya  Ujasiriamali   Mijini & Vijijini , (  EUMIVI  PROJECT ) kwamba  mradi   utazinduliwa  rasmi  siku  ya   Jumamosi  ya  tarehe  01  Septemba   2012,   kuanzia  saa  nne  kamili  asubuhi   katika    eneo  la  Shule   Ya  Msingi  Mlimani  iliyopo  katika   eneo  la   Chuo  Kikuu  Cha  Dar  Es  salaam. Mambo  yatakayo  fanyika   katika  siku  ya  uzinduzi  ni  pamoja  na  kuutambulisha  rasmi  mradi  na  kuanza  kutoa  mafunzo...

Mitaala shule za msingi inawachanganya wanafunzi – Walimu

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Lwengera Darajani, wakiwa wakati wa mapumziko   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitopeni kutoka Wilaya ya Korogwe.   Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitopeni ya Mjini Korogwe, akizungumza na mwandishi wa habari hii   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Lwengera Darajani, wakiwa wakati wa mapumziko BAADHI ya walimu wa shule za msingi wilaya za Korogwe na Moshi wamelalamikia mabadiliko ya mara kwa mara ya mitaala kwa shule za msingi pamoja na idadi kubwa ya masomo kwa wanafunzi wa madarasa ya chini, kuwa yamekuwa yakiwachanganya wanafunzi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni walisema mabadiliko ya mara kwa mara kwa mitaala yanayofanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi bila maandalizi yamekuwa chanzo cha vikwazo cha kufanya vizuri kwa sekta hiyo. Akizungumza hivi karibuni na mwandishi wa habari hizi, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Gerezani, mjini Moshi, Khadija Mtui alisema mabadi...

BAJETI YA ELIMU TANZANIA, 2012/2013 ITAMALIZA AU KUPUNGUZA KERO HIZI?

Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Isensa ya wilayani Nkasi wakiwa darasa, darasa hili lina wanafunzi 211, mwalimu hana pa kukaa akifundisha hutoka nje kusubiri watoto wamalize kuandika. Shule ya msingi Selous iliyopo Namtumbo. Wanafunzi wa darasa la tano wakiwa darasani na mwalimu akifundisha. Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini. Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini. BAJETI ya elimu itasomwa bungeni siku ya Jumatatu, 13 Agosti 2012. Wakati bajeti ya Elimu inasubiriwa kwa hamu na wadau na hasa wapenda maendeleo ya Elimu, Baadhi ya maeneo nchini bado yanakabiliwa na changamoto kubwa sana hasa hali mbaya ya miundombinu, ukosefu wa vyumba vya madarasa na majengo ya shule ambayo yamesababisha baadhi ya shule kuweka madarasa ya nyasi kam...

NAFASI ZA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

RafikiElimu   Foundation     wanatangaza  nafasi za  mafunzo  ya  ujasiriamali .  Mafunzo  yatakayo  tolewa  ni  pamoja  na  : 1.   Kutengeneza  sabuni 2.  Kutengeneza    chaki 3.Kutengeneza  mishumaa. 4.Kutengeneza   viatu  vya  ngozi. 5. Kutengeneza  mkaa  kwa  makaratasi. 6. Kutengeneza  batiki. 7. Uokaji  mikate 8. Usindikaji  wa   vyakula  na  vinywaji  pamoja  na 9.  Uongozi  wa   biashara. WALENGWA   WAKUU  WA  MAFUNZO /  SIFA  ZA   WASHIRIKI Ili  uweze  kupata   nafasi  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  unatakiwa  uwe  na  sifa  zifuatazo: 1.  Uwe  raia  wa  Tanzania. 2. Uwe  na  umri  wa  kuanzia  mia...