Uongozi wa RafikiElimu Foundation, unapenda kuwa julisha wajasiriamali wote walio jiandikisha katika Mradi Wa Mafunzo Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini, ( EUMIVI PROJECT ) kwamba mradi utazinduliwa rasmi siku ya Jumamosi ya tarehe 01 Septemba 2012, kuanzia saa nne kamili asubuhi katika eneo la Shule Ya Msingi Mlimani iliyopo katika eneo la Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam.
Mambo yatakayo fanyika katika siku ya uzinduzi ni pamoja na kuutambulisha rasmi mradi na kuanza kutoa mafunzo rasmi. Kwa wewe uliye jiandikisha unaombwa kufika na kitambulisho chako, kalamu, pamoja na daftari.
Majina Ya Wajasriamali wote wa jijini Dar Es salaam walio jiandikisha katika awamu ya kwanza ya mradi huu yatatolewa rasmi siku ya kesho, yani tarehe 28 Agosti 2012 ( ambayo ndio siku ya mwisho kujiandikisha katika mafunzo ) saa kumi kamili jioni hapa hapa katika tovuti yetu... Kwa wajasiriamali wa mikoani mtapewa taarifa rasmi kuhusu mafunzo siku ya kesho ( tarehe 28 Agosti 2012 ) ifikapo saa kumi kamili alasiri. Vilevile waombaji wote mtatumiwa ujumbe mfupi wa maneno, kuwaita katika mafunzo.
Kufika katika eneo la Shule Ya Msingi Mlimani, kama unatokea Ubungo au Mwenge , panda gari za Ubungo Chuo Kikuu, shuka kituo cha magari kinaitwa UDASA, ukifika hapo UDASA utamkuta mtu ambaye atakupokea na kukuelekeza kilipo kituo cha mafunzo.

Comments
Post a Comment