Skip to main content

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe.
UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa  kama  changamoto  kwa  wajasiriamali
wengi  nchini.


MCHELE.

MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  UNGA  LISHE.

* Karanga    - Nusu  Kilo.
* Soya         - Nusu  Kilo.
* Ulezi         -   Kilo  moja  na  Nusu.
* Mahindi    -Nusu  Kilo
*Mtama     - Mtama  Nusu  Kilo.
* Uwele     -  Nusu  kilo.
* Mchele    -  Nusu  kilo..

JINSI  YA  KUTENGENEZA  UNGA  LISHE.

1. Safisha  ulezi  na  kuutoa michanga  pamoja  na  vumbi.
2. Kaanga  soya  kwenye  moto  mpaka  ibadilike rangi  na  kuwa  " brown "  ama  kahawia.
3. Kaanga  karanga  zako  na  toa  maganda.

Saga  mchanganyiko  wa   malighafi  zote  hapo  juu  kwa  pamoja,  kisha  anika  juani  mpaka  ukauke, halafu  weka  kwenye  vifungashio  kwa  ajili  ya  kuuza.

MASOMO  YA  KESHO  :  Utengenezaji  wa  Chilli  Souce, Tomato  Souce, Mango  Pickles,  Keki,  Soya  Masalla, Wine  Ya  Ndizi, Wine  Ya  Nanasi,  Wine  Ya  Rossela,   Crips  za  Ndizi,   Siagi  Ya  Karanga "  Peanut  Butter ',  Chaki,  Kiwi &  Mkaa  Kwa  Kutumia  Makaratasi  na  Vifuu  vya  Nazi.

ENDELEA  KUTEMBELEA  BLOGU  HII, MARA  KWA  MARA  KWANI  TUTAKUWA  TUKICHAPISHA  MASOMO  YA  UTENGENEZAJI  WA  BIDHAA  ZOTE AMBAZO  TUMEZITANGAZA  KATIKA  MATANGAZO  YETU  YA  AWALI  PAMOJA  NA  NYINGINE  ZA  NYONGEZA  AMBAZO  HATUJA  ZITANGAZA..  KAMA  UNA  SWALI  LOLOTE LILE, MAONI, USHAURI  AMA  UNA  BIDHAA  YOYOTE  AMBAYO  UNGEPENDA  TUIWEKE  HAPA  BLOGUNI  TAFADHALI  WASILIANA  NASI  KWA  :  rafikielimutanzania@gmail.com.

Comments

  1. Asante sana kwa elimu hiyo Mungu akubariki.
    Wataalamu wa afya wanatushauri kutoweka Karanga kwenye mchanganyiko wa lishe kwani Karanga huaribika mapema.katika hilo unashaurije?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Karanga haitakiwi kuchanganywa katika unga lishe wa watoto chini ya mwaka mmoja..
      Ila kama utaaitaka kuitumia waweza kuisaga pembeni na kuiongeza wakati uji ukishaiva

      Delete
  2. Enter your comment...Naomba kujua kwanini baadhi ya washauri wa lishe kw watoto wadogo wanashauri kwamba tusichanganye nafaka zingine na karanga?

    ReplyDelete
    Replies
    1. hautakiwi kuchanganya nafaka zaid ya mbili katika unga lishe wa watoto kwa sababu zifuatazo..
      1.Mfumo wa mmengenyo wa mtoto unakuwa haujakomaa vyema kuweza kumengenya vyakula vyote kwa usahihi hivyo humsababishia mtoto matatizo ya kupata choo kigumu.
      2.Nafaka zinapokuwa zaidi ya mbili huwa ni ngumu kujua kama kama uji umeiva kwa usahihi na husababisha uji kuwa mmbichi kwa sababu kila nafaka huiva katika viwango tofauti na pia kama utauupika uji huo kwa muda mrefu husababisha kupoteza baadhi ya virutubisho.

      Delete
    2. Tena Mbaya Zaidi kachakugua ulezi Kwa wingi ambao una makapi mengi na vigumu kumeng'enywa na watoto! Tutaharibu watoto wa watu kama huna Elimu ya Lishe tulia tu usilazimishe

      Delete
  3. ,,,blessaaap guys,
    I think we must cling on those excellent knowledgeable ideas!!

    ReplyDelete
  4. ,,,blessaaap guys,
    I think we must cling on those excellent knowledgeable ideas!!

    ReplyDelete
  5. Asante kwa somo hili zuri. Nami ningependa kujua kutoka maswali yaliyoulizwa hapo juu.

    ReplyDelete
  6. Mmmmmmmmmh kwaiyo soya sio lazma kuchemsha na kutoa maganda

    ReplyDelete
  7. Kwan karanga na soya ukizikaanga virutubisho havitoki maana ulishaivisha

    ReplyDelete
  8. Mchanganyiko gani kati ya hizo nafaka huweza kutoa lishe bora zaid

    ReplyDelete
  9. ukitumia mahindi kg 10 kwaajili ya biashara , mbegu za maboga,soya ,ulezi na mchele unatakiwa kutumia kiasi gani

    ReplyDelete
  10. Tayari umeshawapotosha watu. hakuna sababu ya msingi ya kuchanganya nafaka zaidi ya moja

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenye  uzito  wa  kg. 5. * Chemsha  kwa  muda  wa  dakika  30  kwa  moto  wa  kawaida (  Inashauriwa  kutumia  moto  wa  mkaa  ) * Baada  ya  kupoa   anza kuchachua  kwa  kuweka  amira   vijiko  vinne (  4  )  vya  chakula ,  sukari  vijiko  viwili  vya  chai na  kisha  koroga  kwa  muda  wa  dakika  20. *  Acha  kwa  muda  wa  dakika  5  ukiwa  una 

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Kisu. *Vikombe 2 vya plasitiki. * Makopo  2  ya plasiki au kaure. Vipimo vinavyo tajwa hapa ni chombo chochote cha plastic ( kama kikombe,kopo n.k.} Vipimo vyote ni vya ujazo na mara zote vikae wi