Nanasi. |
Wine ya nanasi ni rahisi kutengeneza kwa sababu mananasi yanapatikana kwa wingi sana katika kipindi kirefu cha mwaka.
MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA KATIKA UTENGENEZAJI WA WINE YA NANASI.
* Nanasi.
* Maji.
* Sukari.
* Amira.
HATUA YA KWANZA KUTENGENEZA
* Menye maganda ya mananase na kupata nyama . ( Kinacho tumika katika utengenezaji wa wine ya nanasi ni nanasi lenyewe na sio maganda ya mananasi )
* Katakata vipande vidogo kisha weka katika chombo kwa ajili ya kuchemsha, nanasi linalo faa katika utengenezaji wa wine ya nanasi ni nanasi lenye uzito wa kg. 5.
* Chemsha kwa muda wa dakika 30 kwa moto wa kawaida ( Inashauriwa kutumia moto wa mkaa )
* Baada ya kupoa anza kuchachua kwa kuweka amira vijiko vinne ( 4 ) vya chakula , sukari vijiko viwili vya chai na kisha koroga kwa muda wa dakika 20.
* Acha kwa muda wa dakika 5 ukiwa una koroga kila siku.
HATUA YA PILI.
Baada ya siku tano kukamilika, chuja wine yako iweke katika chombo cha kupunguza gesi kwa muda wa siku 21. Baada ya siku 21 , wine yako itakuwa tayari, unaweza kui hifadhi kwa ajili ya matumizi.
Comments
Post a Comment