Maandalizi ya utengenezaji wa Tomato Souce. |
Tomato Souce. |
MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA KWENYE UTENGENEZAJI WA TOMATO SOUCE.
1. Nyanya Kg 1.5 ( Kilo moja na nusu )
2.Vitunguu Maji. Vitatu vilivyo menywa na kukatwa katwa vipande.
3. Mafuta ya Kupikia Vijiko Sita Vya Chakula.
4. Sukari Vijiko viwili vya chai.
5. Citric Acid.
6.Vinegar. Vijiko viwili vya chai.
HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA UTENGENEZAJI WA TOMATO SOUCE.
Tomato Souce iliyo katika hatua za maandalizi |
1. Saga mchanganyiko wa malighafi zote zilizo tajwa hapo juu kwa pamoja kwa kutumia mashine ya blender mpaka uwe rojo rojo.
2. Tenga jiko la mkaa lenye moto wa wastani, kisha injika kikaangio kwenye moto halafu weka mafuta ya kupikia vijiko sita vya chakula.
3. Mafuta yakianza kuchemka , anza kumimina mchanganyiko wako huo ndani ya kikaango hicho huku ukiwa una koroga upande mmoja mpaka umalize kuchanganya. Tumia dakika 15 kufanya zoezi hili.
* Utakapo ona mchemsho wako umeanza kuwa uji uji, ipua na weka kwenye chombo safi tayari kwa matumizi.
Citric Acid inatakiwa kiasi gani ili kuweka uwiano ulio sahihi bila kuasili afya za watumiaji?
ReplyDelete