MASOMO YATAKAYO FUNDISHWA HAPA NI :
11. Utengenezaji Wa Sabuni isiyo na garama.
22. Utengenezaji Wa Sabuni ya urembo.
33. Utengenezaji Wa Sabuni ya asali na cream.
44. Utengenezaji Wa Sabuni
ya manukato.
55. Utengenezaji Wa Sabuni
ngumu.
66. Utengenezaji Wa Sabuni
ya unga
77. Utengenezaji Wa Sabuni ya kugandisha.
88. Utengenezaji Wa Sabuni
za dawa.
99. Utengenezaji Wa Sabuni
za rangi.
110. Utengenezaji Wa Cream ya kunyolea.
111. Utengenezaji Wa Sabuni iliyotengenezwa na mafuta
mengine.
VIFAA VYA UTENGENEZAJI
SABUNI.
*Sufuria.
*Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki.
*Mafuta
*Maji.
*Sodium hydroxide{NaOH}
*Ubao mdogo/mwiko.
*Chombo chenye ukubwa cha plastiki.
*Kifyatulio.
*Kisu.
*Vikombe 2 vya plasitiki.
* Makopo 2 ya plasiki au kaure.
Vipimo vinavyo tajwa hapa ni chombo chochote cha plastic (
kama kikombe,kopo n.k.}
Vipimo vyote ni vya ujazo na mara zote vikae wima.
TAHADHARI-
Sodium hydroxide {NaOH} ni hatari.
Lazima iwekwe mbali na mahali
wanakofikia watoto.
*Kama mtoto atameza sodium
hydroxide ni lazima apewe maziwa mengi au kikombe 1 cha mchanganyiko wa juisi
ya limau/siki na vikombe 20 vya maji.
*Sodium hydroxide hushambulia ngozi,
kuwa mwangalifu kila mara unapotengeneza sabuni, nawa mikono vizuri, hali
ya unyevu katika hewa huibadili sodium
hydroxide kuwa kimiminika hivyo ni rahisi kudhuru ngozi yako.
*Sodium hydroxide hushambulia aina
zote za metali, hivyo tumia vyombo vya mfinyanzi hii itasaidia na kama
vyombo vya mfinyanzi
havipatikani tumia aina nyingine ya vyombo vya plastiki.
Ni lazima sodium hydroxide
{NaOH} ihifadhiwe vizuri kwenye vyombo visivyopitisha hewa.
1. SABUNI ISIYO NA GHARAMA
Utengenezaji wa sabuni hii
unahitaji juhudi na kazi kubwa kwa mtengenezaji.
Jinsi ya kutengeneza –
Hatua ya 1
*Kusanya maganda ya ndizi, magogo ya
mipapai, maganda ya mbegu za kakao, kausha vitu hivi kwenye jiko la jua hadi
vikauke, kama huna jiko la jua vikaushe juani.
Hatua ya 2
*Vichome hadi kupata jivu, pia
unaweza kutumia jivu la kuni au karatasi ambazo hazijaandikwa na
sii jivu la plastiki au vitu visivyo vya asili.
*Kusanya majivu na uyapima kwenye
ndoo ya lita 10.
*Tumia ndoo yenye ujazo wa lita 20,
ongeza lita 15 za maji ya moto na Koroga vizuri, baada ya dakika
10, chuja kwa kutumia kitambaa, Kumbuka wakati wote kutumia ndoo ya plastiki au
chombo cha mfinyanzi.
*Ongeza maji ya moto lita 5 kwenye
majivu yaliyobaki endelea kukoroga kwa dakika 10 halafu chuja tena.
*Weka pamoja vile vyote ulivyochuja
kwenye chombo cha mfinyanzi kama utatumia chombo cha metali kitaharibika.
Hatua ya 3
*Chemsha mchanganyiko wako hadi
ubakie kikombe 1tu au ml 200 ongeza kikombe kimoja cha mawese halafu chemsha
tena kwa muda mfupi, kuwa makini wakati wa kufanya kitendo cha kuongeza mafuta
kwani mchanganyiko huu hutoa povu jingi.
Hatua ya 4
*Mimina mchanganyiko wako kwenye
kifyatulio na acha ikauke, iweke majuma 8 hadi 12 na hapo itakuwa tayari kwa
kutumia.
2. SABUNI YA UREMBO
Sabuni hizi zinatengenezwa na mafuta
safi na ni nzuri sana kwa ngozi ya mwili.
Unapotumia sabuni hizi ngozi yako
hungara kwa sababu ya tabia yake ya kuufanya mwili kama umepakwa mafuta kila
wakati.
Mahitaji –
*Mafuata ya mbogamboga/ mawese
vipimo 8
*Maji vipimo 5.
*Sodium hydroxide {NaOH}kipimo
1
JINSI YA KUCHANGANYA
Hatua ya 1
Pima maji vipimo 5, ongeza sodium
hydroxide {NaOH} kipimmo 1, koroga mchanganyiko huo na uache hadi joto lake
lipungue.
Hatua ya 2
*Ongeza mafuta vipimo 8 kwenye
mchanganyiko wako huku ukikoroga bila kusita kwa muda usiopungua dakika 60, ili
kuutambua kama mchanganyiko wako umekuwa tayari utaona umekuwa laini.
Hatua ya 3
*Mimina kwenye trea au vifyatulio,
kabla sabuni haijawa ngumu unaweza kukata kwa maumbo unayotaka au kutia urembo,
jina kwenye sabuni huu ndio wakati muafaka.
*hifadhi sabuni mahali penye mwanga
na penye kivuli, ni lazima sabuni ikaae majuma 8 hadi 12 au ianikwe kwenye jiko
la jua kwa majuma 3 hadi 4 kabla ya kutumika.
Kuharakisha kuitumia ni hatari kwa
sababu sodium hydroxide itakuwa haijamaliza utaratibu wa utengenezaji hivyo
kuharibu ngozi ya mtumiaji.
3.SABUNI YA MANUKATO
Mahitaji –
*Unga wa sabuni
iliyotengenezwa na kuwa tayari zaidi ya majuma 8
*Maji
Jinsi ya kutengeneza-
Hatua ya 1
*Saga sabuni iliyotengenezwa muda
mrefu kupata unga.
Pima vipimo 8 vya unga wa
sabuni, ongeza maji vipimo 2 na yeyusha kwenye joto la kadiri huku ukikoroga
hadi utakapo changanyika vizuri.
Hatua ya 2
*Ongeza matone mawili ama matatu ya
marashi halafu mimina kwenye vifyatulio.
*Usiwe na haraka unapotengeneza
sabuni za manukato kama hutotumia njia niliyokuonyesha hapo juu sodium
hydroxide itaharibu manukato uliyoweka.
.
4. SABUNI YA ASALI AU CREAM
*Mafuta vipimo 8.
*Maji vipimo 5.
*Sodium hydroxide kipimo 1.
*Asali kipimo 1.
Sabuni hii inatengenezwa kama
sabuni namba 2 lakini baada ya kuchanganya vitu vyote unaongeza kipimo 1
cha asali.
5.
SABUNI NGUMU
Sabuni hii inatumika kuondoa
uchafu mgumu
Pima maji vipimo 5 ongeza sodium
hydroxide kipimo 1acha mchanganyiko uchanganyike vizuri hadi uanze kupoa.
Ongeza mafuta vipimo 6 kwenye mchanganyiko wako huku ukikoroga bila kukoma hadi
dakika 60.
Kabla sabuni haijawa ngumu sana,
ongeza vipimo 2 vya kaolin iliyochekechwa vizuri kama kaolini haipatikani
unaweza kutumia majivu ya kuni yaliyochekechwa vizuri mimina sabuni kwenye
kifyatulio na baada ya kuganda ikate vipande kasha iweke sehemu safi ikauke
taratibu hadi ndani ya wiki 12 sabuni itakuwa tayari kutumika.
Sabuni hii ni ile inayotumiwa na
watu kwa ajili ya kufulia hii inafaa sana hasa katika maeneo yaliyo na
maji chumvi.
Utengenezaji wake hautofautiani sana
na sabuni nyingine lakini sabuni hii ina mawese au mafuta kidogo kuliko zile za
kuogea au za kipande.
Maji
vipimo 4
Sodium hydroxide {NaOH} kipimo1
Mafuta
vipimo 5
Baada ya kuchanganya na kuikoroga
kwa muda wa dakika 60 acha ikauke kama sabuni nyingine muda usiopungua majuma 8
hadi 12, isage na kuichekecha na chekecheo ili kupata unga laini wenye ukubwa
ulio sawasawa hapo sabuni yetu iko tayari kuifungasha na kuiingiza sokoni ama
kuitumia wewe mwenyewe.
7. SABUNI YA KUGANDISHA
Utengenezaji wa sabuni hii una njia
nyingi
Njia ya kwanza
Hatua ya kwanza –
Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya
mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye
chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki.
Hatua ya pili-
Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye
chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa
kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke.
Subiri mchanganyiko wa sodium
hydroxide na mafuta ukaribie kupoa.
Hatua ya tatu-
Taratibu ongeza mchanganyiko wa
sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha
ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi.
Njia ya pili
{a}Chemsha mafuta kwenye joto la
kadiri ya 55C
{b}Changanya maji na sodium
hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo.
.{c}baada ya kuandaa mchanyiko wako
changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo,
taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni
ndani ya kasha la mbao lilotangulizwa karatasi nyembamba la plastiki subiri saa
3 na sawazisha sabuni kwa rula au kitu kingine kilicho nyooka huku ukigandamiza
juu, ipanguse iwe laini kwa kutumia kitamba kilicho lowanishwa.
{g}katakata sabuni vipande kwa
kipimo cha kuuza iweke ikauke katika sehemu yenye kivuli kwa muda wa majuma 8
hadi 12 mfano- ndani ya chumba kwenye sakafu iliyotandikwa kasha la karatasi
nene.
8.SABUNI YA DAWA
Sabuni hii inahitaji vitu
vifuuatavyo
Unga wa sabuni iliyotengenezwa zaidi
ya wiki 8 vipimo 4
Mafuta ya dawa yaliyotengenezwa na
unga wa dawa uliotokana na miti ya dawa kama moringa,mwarubaini
n.k
kipimo 1 kama mafuta haya hayapatikani unaweza ukatumia unga wenyewe.
Maji
kipimo 1
Jinsi ya kutengeneza-
Changanya vitu vyote kwa pamoja huku
ukikoroga mchanganyiko huo kwenye joto la kadiri hadi mchanganyiko uchanganyike
vizuri kisha mimina mchanganyiko huo kwenye kifyatulio subiri hadi ipoe na
kugande.
Baada ya sabuni kuganda kata kwa
umbo unalolitaka kwa kutmia kifaa ulichokiandaa kama kisu,kibati n.k ili kupata
vipande vilivyo lingana.
9. SABUNI YA RANGI KWA KUTUMIA VITU ASILIA
Sabuni hizi ni zile ambazo
zinatengenezwa na rangi asilia ambazo hazina mazara yoyote kwenye ngozi
ya binadamu
Unaweza kujiuliza ni kwa jinsi gain
nitapata rangi ya sabuni huku sina fedha ya kununua hii sii tatizo tumia rangi
za viungo kama manjano, zingifuri,karafuu, unga wa miti ya dawa kama
mwarubaini,mronge na hata mafuta ya mawese.
Kitendo cha kuweka rangi kwenye
sabuni unaamua uweke wakati gaini wakati unaanza au wakati wa kumalizia hii
haina tatizo ila nategemea.
mafuta ya mawese huwa na rangi ya
njano ,nyekundu kutokana na carotene iliyomo.
Kwa sababu hii ukitumia mawese bila
kuharibu carotene iliyopo unapata sabuni ya njano na hii ni rangi halisi na ya
asili isiyo na madhara yoyote.
Mawese pamoja na mbegu za bixa hupata
sabuni nyekundu.
10. CREAM YA KUNYOLEWA
MAHITAJI
Majani mabichi yanayo nukia mfano
mkaratusi, limau, michaichai, lavenda
kipimo 1
Maji
kipimo 1
Unga
wa sabuni iliyotengenezwa zaidiya wiki 8 vipimo 5
Asali
kipimo 3
Changanya
vitu hivyo kwa pamoja taratibu chemsha mchanganyiko huu hadi uwe kitu kmoja,
hii ni nzuri ikifanyika kwenye jiko la jua itasaidia kupunguza kiwango cha
mvuke utakao toweka wakati wa kuchemsha.
Kama
huna jiko la jua basi lazima uongeze maji ili kurudisha katika ujazo wa awali,
baada ya kuepua koroga hivyo hivyo wakati inaendelea kupoa, ikisha poa kabisa
hifadhi katika chombo kisichopitisha hewa ili kuzuia isikauke.
chombo
kizuri ni cha kioo, plastiki au kaure.
11. SABUNI ILIYOTRENGENEZWA NA MAFUTA MENGINE.
Kama utatumia mafuta ya aina
nyingine mfano ya shahamu au mafuta ya karanga hapa utengenezaji utakuwa mgumu
zaidi.
Jinsi ya kutengeneza - yeyusha
sodium hydroxide kwenye ml 200 za maji ongeza gr 200 za shahamu huku
ukikoroga ongeza gr 600 za maji ya moto baada ya mchanganyiko
kuchanganyika vizuri hifadhi mchanganyiko kwenye joto la 70 hadi80C angalau kwa
saa 6 kwenye jiko la jua koroga kila baada ya dakika 15 kisha ongeza
mchanganyiko wa chumvi ya kawaida gramu120 na maji ml200.
Acha mchanganyiko upoe hapo sabuni
itatuama juu ya maji kasha mimina sabuni kwenye kifyatulio na iache ikae miezi
miwili hadi mitatu ili ikauke vizuri.
Sabuni ulizotengeneza nyumbani ni
nzuri kuliko zilizotengenezwa viwandani.
Maana ya maneno
Kaolingi ni
udongo mweupe wa mfinyanzi unaopatikana mtoni. katika Africa hutumika
kupamba kuta za nyumba .
Sodium hydroxide
NaOH ni kastiki.
Shahamu ni
mafuta ya wanyama kama mafuta ya ngombe,kondoo, nk.
Good article
ReplyDeleteNice ,but ukisema vipimo unamaanisha mini kijiko au Lita
ReplyDeleteni elimu nzuri kwa jamii
ReplyDeleteVERY NICE
ReplyDeleteVERY NICE
ReplyDeleteNaomba kujua material ya sabuni za kipande yanakopatikana
ReplyDeleteSafi sana aisee
ReplyDeletevery nice! Ila nahitaji kujua maana ya kipimo
ReplyDeletevery nice! Ila nahitaji kujua maana ya kipimo
ReplyDeleteunavyosema sabuni iliyotengezwa zaidi ya wiki nane unamaanisha naweza nikatumia sabuni za kawaida za madukani au?
ReplyDeleteKipimo ni nini mpendwa
ReplyDeleteVipimo. ni vikombe au. kitu gani
ReplyDeleteAsante sana kwa elimu nzuri. Kipimo ina maana gani? Au ina maana kifaa chochote nitakachotumia kupimia? Je ni cha uzito au cha ujazo?
ReplyDeleteHabari,naweza kupata namba zenu za simu?
ReplyDeleteno somo zuri, je malighafi kwa huku wilayani zinapatikana wap na kwa gharama ya beo gani?
ReplyDelete