Skip to main content

SOMO LA SITA : UTENGENEZAJI WA MANGO PICKLES



Mango  Pickles



 MANGO  PICKLES    au    "  ACHARI  YA  EMBE  "  ni  chachandu  inayo  tumika  kunogesha  utamu  wa  chakula.   Malighafi  kuu  katika  utengenezaji  wa  "  MANGO  PICKLES "  ni  embe.

                                  MATAYARISHO

* Embe  zisafishwe  vizuri  kwa  kuosha  vizuri  kwa  kutumia  maji  masafi.
( Embe  zioshwe kabla  hazijamenywa )

* Embe  likatwe  katwe  vipande  bila  kuligusa  kokwa,  vipande  hivyo  viwekwe  kwenye  kichanja  baada  ya  kukatwa  katwa  na  vianikwe   juani  kwa  muda  wa  nusu  saa.

*  Hifadhi  embe  zako  hizo  kwenye  chombo  kisafi, kwa  muda  wa  siku  tano.


                     KUTENGENEZA  MANGO  PICKLES

* Tayarisha  nyanya  robo  kilo, menya  maganda  na  katakata  vipande  vidogo.

* Katakata  vitunguu    viwili   vikubwa.

* Chumvi   vijiko  viwili  vya  chai.

* Vinegar  _  kijiko  kimoja  cha  chai  kwa  ajili  ya  kuifanya  mango  pickle  yako  isiharibike.

* Maji  ya  limao  vijiko  viwili  vya  chai.

Tengeneza   rosti  ya  mchanganyiko  wa  malighafi  zote  zilizo  tajwa  hapo  juu. Baada  ya  kutengeneza  rosti  hiyo, chukua  vipand  vyako  vya  embe na  changanya  na  rosti  yako.

Weka  vipande  vyako  vya  embe  ndani  ya  rosti  hii, kisha  hifadhi  katika   kifungashio  kwa  ajili  ya  matumizi ..

N.B:  Kwa  kiwango  hiki  cha   rosti  una shauriwa  uweke   vipande  vya  embe  vyenye  uzito  wa  kilo  moja.  

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa  kama  changamoto  kwa  wajasiriamali wengi  nchini. MCHELE. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  UNGA  LISHE. * Karanga    - Nusu  Kilo. * Soya         - Nusu  Kilo. * Ulezi         -   Kilo  moja  na  Nusu. * Mahindi    -Nusu  Kilo *Mtama     - Mtama  Nusu  Kilo. * Uwele     -  Nusu  kilo. * Mchele    -  Nusu  kilo.. JINSI  YA  KUTENGENEZA  UNGA  LISHE . 1. S

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenye  uzito  wa  kg. 5. * Chemsha  kwa  muda  wa  dakika  30  kwa  moto  wa  kawaida (  Inashauriwa  kutumia  moto  wa  mkaa  ) * Baada  ya  kupoa   anza kuchachua  kwa  kuweka  amira   vijiko  vinne (  4  )  vya  chakula ,  sukari  vijiko  viwili  vya  chai na  kisha  koroga  kwa  muda  wa  dakika  20. *  Acha  kwa  muda  wa  dakika  5  ukiwa  una 

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Kisu. *Vikombe 2 vya plasitiki. * Makopo  2  ya plasiki au kaure. Vipimo vinavyo tajwa hapa ni chombo chochote cha plastic ( kama kikombe,kopo n.k.} Vipimo vyote ni vya ujazo na mara zote vikae wi