UONGOZI wa Taasisi Ya RAFIKIELIMU FOUNDATION unapenda kuwafahamisha wanafunzi wote walio jiandikisha katika mafunzo ya ujasiriamali yanayo tolewa na taasisi yetu kupitia Mradi wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini " EUMIVI Project " kwamba kuanzia leo tarehe 12 NOVEMBA 2012, masomo ya UZALISHAJI & UTENGENEZAJI wa bidhaa mbalimbali kwa njia ya NADHARIA yatakuwa yakitolewa online kupitia katika blogu yetu hii. Uamuzi huu umetokana na maombi ya watu wengi . Utaratibu utakuwa kama ifuatavyo; kila siku tutakuwa tunatoa somo moja au masomo mawili au zaidi, kulingana na nafasi yetu pamoja na ukubwa wa somo husika. Jukumu lako litakuwa ni kuyafuatilia masomo hayo na kuyafanyia kazi.
UTARATIBU WA MAFUNZO KWA NJIA YA VITENDO :
Kama tulivyo toa maelezo yetu katika semina zetu mbalimbali, mafunzo kwa vitendo yatakuwa yakifanywa kwa makundi ya mawili mawili, kila kundi likiwa na watu ishirini.
Jukumu lako wewe kama mwanafunzi, wa EUMIVI ni kutafuta watu kwa ajili ya kuunda makundi ya kufanya mafunzo kwa vitendo. Hii ina maana kuwa kila mwanafunzi wa EUMIVI anatakiwa kuwa kiongozi wa kundi ama makundi ya watu atakao waandikisha katika mradi. Isisahaulike kuwa, malipo ya " commission " ya shilingi elfu moja kwa kila mtu utakaye muandikisha katika mradi yapo pale pale.
KUMBUKA : JUHUDI zako wewe kama mwanafunzi wa EUMIVI , ndio zitakazo kufanya upate nafasi ya kuhudhuria mafunzo kwa vitendo. Endapo utashindwa kutengeneza kundi la angalau watu ishirini au zaidi kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo kwa vitendo, basi amini nakwambia hutoweza kupata nafasi ya kuhudhuria hayo mafunzo ya vitendo yanayo tolewa bure kabisa na taasisi yetu kupitia mradi huu.
UNACHO TAKIWA KUFANYA : Unacho takiwa kufanya ni kuwaandikisha watu angalau ishirini , na kutuma majina yao kwetu kwa njia ya barua pepe, then sisi tutakutafutieni tarehe kwa ajili ya kufanya hayo mafunzo ya vitendo.
TUNAOMBA USHIRIKIANO KUTOKA KWENU.
ASANTENI.

Comments
Post a Comment