|
Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Isensa ya wilayani Nkasi wakiwa darasa, darasa hili lina wanafunzi 211, mwalimu hana pa kukaa akifundisha hutoka nje kusubiri watoto wamalize kuandika. |
|
Shule ya msingi Selous iliyopo Namtumbo. Wanafunzi wa darasa la tano wakiwa darasani na mwalimu akifundisha. |
|
Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini. |
|
Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini. |
BAJETI ya elimu itasomwa bungeni siku ya Jumatatu, 13 Agosti 2012. Wakati bajeti ya Elimu inasubiriwa kwa hamu na wadau na hasa wapenda maendeleo ya Elimu, Baadhi ya maeneo nchini bado yanakabiliwa na changamoto kubwa sana hasa hali mbaya ya miundombinu, ukosefu wa vyumba vya madarasa na majengo ya shule ambayo yamesababisha baadhi ya shule kuweka madarasa ya nyasi kama Shule ya Msingi Selous na shule ya Msingi Mkapa zilizopo wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma, Shule ya Msingi Silabu iliyoko wilayani Korogwe, mkoani Tanga na Shule ya msingi Misunkumilo ya wilayani Nkasi,mkoani Rukwa pamoja na baadhi ya shule wilayani Muleba na Tanzania nzima kwa ujumla.
|
Shule hii ipo wilayani Muleba. |
Hali ya elimu imezidi kuwa mbaya kila kukicha, kiasi kwamba hata watu hudiriki kuuliza kama shule hizo zipo nchini, hasa wakiangalia juhudi na kelele nyingi zilizopigwa juu ya mchango mkubwa wa MMEM na MMES kuwa zimefanya kazi kubwa sana kuboresha mazingira ya kujifunzia hasa miundombinu ya shule. Swali Je, shule hizi ziliachwa wapi na mipango hii? Je bajeti ya elimu ya 2012/2013 itatatua baadhi ya changamoto za elimu nchini?na kuondokana na majengo haya yasiyo rafiki kwa mwanafunzi na mwalimu?
|
? Hiki ni choo cha Shule ya Msingi iliyopo wilayani Muleba, mkoani Kagera. Ni msingi upi tunaojengea watoto wetu kama wanajifunza katika mazingira yasiyo rafiki kama haya? |
Hebu angalia jinsi ambavyo wanafunzi huko Tanga, Rukwa, Kagera na Ruvuma wanavyojifunza kwenyesehemu zinazokatisha tamaa: Wataweza kweli? Mungu Ibariki Tanzania , Mungu Ibariki Afrika!
Comments
Post a Comment