Taasisi ya RafikiElimu Education Consultancy, kupitia Mradi wa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa njia ya videon( VIDEO - MAFUNZO PROJECT) inakutangazia wewe kijana wa ki Tanzania, nafasi ya kujiunga na mafunzo ya Ujasiriamali kwa njia ya video.
Masomo yatakayo fundishwa ni pamoja na 👇
1. Jinsi ya kutengeneza pipi za kihindi ( Pipi za Kihindi) ni pipi zinazo tengenezwa Nyumbani kwa kutumia sukari ya kawaida ama sukari guru. Pipi hizi ni pipi zinazo pendwa Sana na watoto wa shule za msingi na sekondari. Kijana akijua jinsi ya kutengeneza pipi hizi, anakuwa amepata ujuzi utakao muwezesha kujitengenezea kipato chake halali kupitia kutengeneza pipi hizo za kihindi na kwenda kuziuza mashuleni
2. Jinsi ya kutengeneza mashine za kutotolea vifaranga wa kuku ( Incubators)
3. Jinsi ya kutengeneza chaki.
4. Jinsi ya kutengeneza sabuni za aina mbalimbali.
5. Jinsi ya kutengeneza ice cream, na juice za aina mbalimbali.
6. Pamoja na masomo mengine mengi.
Mafunzo haya yanatolewa kwa njia ya video, hivyo unaweza kuyapata mahali popote pale ulipo ndani na nje ya Tanzania.
Mafunzo yataanza Kutolewa rasmi siku ya Jumatatu ya tarehe 4 AGOSTI 2025.
FOMU ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO HAYA ZINAPATIKANA OFISINI KWETU CHANIKA MWISHO ( NZASA KWA MWARABU)
Kwa wewe ulie mbali na CHANIKA au ulie nje ya Dar Es Salaam, tuandikie barua ya maombi ya fomu ya kujiunga na mafunzo haya kupitia barua Pepe yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.com.
Au kupitia WHATSAPP number:
0745 433 595.
Mwisho wa kupokea maombi ya fomu za kujiunga na mafunzo haya ni siku ya Juamatatu ya tarehe 01 AGOSTI 2025 saa tisa kamili alasiri.
Kwa taarifa zaidi kuhusu mradi huu pamoja na kazi zetu nyingine, tutembelee kila siku hapa hapa kwenye blogu yetu.
Comments
Post a Comment