Skip to main content

MCHAWI NI ENGLISH!!! TUNASIMAMIA MAENDELEO YA SOMO LA KIINGEREZA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI

 

MCHAWI NI ENGLISH!!!

TUNASIMAMIA MAENDELEO YA SOMO LA KIINGEREZA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI

Wanafunzi wengi wa shule za sekondari nchini, hushindwa kufanya vizuri kwenye masomo yao ya sekondari , kwa sababu ya kukosa msingi mzuri wa somo la kiingereza tangu shule ya msingi. Kukosa msingi mzuri wa somo la kiingereza , husababisha wanafunzi kushindwa kuelewa vizuri masomo ya sekondari ambayo hufundishwa kwa somo la kiingereza. Matokeo yake, wanafunzi hao, huishia kufeli vibaya kwenye mitihani yao ya kuhitimu kidato cha nne, sio kwa sababu hawana akili? La Hasha! Sababu ni kutokuelewa vizuri lugha ya kiingereza.  Kwa sababu hiyo basi,  Taasisi ya RafikiElimu EDUCATION Consultancy, imeanzisha program  maalumu ya kuwasaidia wanafunzi wa sekondari kupata msingi bora wa somo la kiingereza ( English) ambao utwasaidia kuelewa vizuri masomo yao, jambo litakalo wasaidia kupata ufaulu mzuri kwenye mitihani yao ya mwisho ya kidato cha nne.

 

Mzazi au mlezi , ambae unatamani kuona mtoto wako akifaulu vizuri kwenye mitihani yake ya kidato cha nne, njoo umuandikishe kwenye program yetu ili tuweze kumsimamia vizuri kwenye somo la kiingereza.  Mbali na kumsimamia kwenye somo la kiingereza, lakini pia tunasimamia maendeleo ya kitaaluma ( masomo yote) kwa wanafunzi walio chini ya program yetu, kwa kuhakikisha  wanapata ufaulu mzuri kwenye mitihani yao ya kuhitimu kidato cha nne. Program yetu hai ingiliani na ratiba yake ya darasani. Gharama ya kujiunga na program hii ni nafuu sana na inalipwa kwa mwezi. Fomu za kujiunga na program hii zinapatikana kwenye ofisi ya tawi letu la Chanika,iliyopo eneo la Nzasa- Kwa Mwarabu. Kufika ofisini kwetu, panda bajaji za Nzasa-Shule kisha shuka Nzasa Kwa Mwarabu , halafu piga simu namba :0693  005 189.

Tovuti : www.rafikielimu.blogspot.com

E.mail: rafikielimutanzania@gmail.com

Instagram : RafikiElimu Education Consultancy

Muandikishe mtoto wako mapema ili aanze program mapema.

 

 

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...