Skip to main content

MPE MWANAO MSINGI MZURI WA SOMO LA KIINGEREZA KABLA HAJAFIKA SEKONDARI

 

MPE MWANAO MSINGI MZURI WA SOMO LA KIINGEREZA KABLA HAJAFIKA SEKONDARI

 


Tunasimamia Maendeleo Ya Somo  La Kiingereza Kwa Watoto Wanao Soma Shule Za Msingi Mtaala wa Kiswahili

 

Wanafunzi wengi wanao feli masomo ya sekondari ni wale ambao walikosa msingi mzuri wa somo la kiingereza walipo kuwa shule ya msingi.  Na hii ni kwa sababu, ukiondoa somo la Kiswahili , masomo mengine yote ya sekondari hutolewa kwa lugha ya kiingereza.  Kama mwanafunzi alikosa msingi mzuri wa somo la kiingereza alipokuwa shule ya msingi, hawezi kuelewa masomo ya sekondari. Matokeo yake, mwanafunzi huyo hufeli kwenye mitihani yake ya kuhitimu kidato cha nne.  Kama mtoto wako hajapata msingi mzuri wa somo la kiingereza akiwa shule ya msingi, hakuna muujiza mwingine wowote unao weza kumfanya aelewe na kufaulu vizuri masomo ya sekondari, zaidi ya kupata msingi mzuri wa somo la kiingereza. Kwa kuzingatia umuhimu wa somo la somo la kiingereza, taasisi ya Rafiki Elimu EDUCATION  Consultancy, imenzisha program maalumu ya kuwasaidia wanafunzi wanao soma shule za msingi kwa mtaala wa lugha ya Kiswahili, kuelewa na kupata msingi bora kabisa wa somo la Kiingereza ( English ). Mtoto atapata program zote za lugha ya kiingereza kama zinavyo tolewa kwenye shule za mtaala wa kiingereza ( English Mediums) ambazo  zinafanya vizuri kitaaluma nchini.  Mzazi unaesomesha mtoto wako kwenye shule ya msingi inayo fuata mtaala wa Kiswahili, na unatamani mtoto wako apate msingi bora wa somo la kiingereza, muandikishe kwenye program yetu.

 

Tutamsimamia vizuri kwenye somo la kiingereza ( English) na tutahakikisha anamaliza darasa la saba akiwa amewiva vizuri sana kwenye somo la kiingereza . Program hii imeandaliwa kitaalamu na imeandaliwa katika namna ambayo haiwezi kuingiliana na ratiba ya masomo yake ya darasani.

 

Gharama ya kujiunga na program hii ni rahisi sana na inalipwa kwa mwezi.  Fomu za kujiunga na program hii zinapatikana kwenye ofisi ya tawi letu jipya ya Chanika, iliyopo katika eneo la NZASA KWA MWARABU. Kufika ofisini kwetu, panda bajaji za NZASA-SHULE , shuka kwa Mwarabu kisha piga simu namba 0693  005  189.

 

Kwa taarifa zaidi kuhusu kazi na program zetu nyingine, tutembelee kupitia :

 

Tovuti yetu : www.rafikielimu.blogspot.com

Barua pepe ( E.mail): rafikielimutanzania@gmail.com

Instagram Page : RafikiElimu EDUCATION Consultancy.

Muandikishe mwanao mapema ili aanze program mapema

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...