Skip to main content

MRADI WA " ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI" WAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

Mwalimu  wa  Ujasiriamali  kutoka  katika  Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation, Mama  Ashankira  Lupembe  , akifundisha  kwa  vitendo  namna  ya  kutengeneza  sabuni   ya  maji.
Mwanafunzi  wa  ujasiriamali  akitengeneza  sabuni  ya  unga  mwenyewe  mara  baada  ya  kupata  maelekezo  kutoka  kwa   waalimu  wa  ujasiriamali  kutoka  RafikiELIMU  Foundation.
Mwanafunzi  wa  ujasiriamali  akitengeneza  sabuni  ya  maji  kwa  vitendo   mara  baada  ya  kupata  maelekezo  kutoka  kwa   waalimu  wa  Ujasiriamali  kutoka  katika  Asasi  ya  RafikiElimu  Foundation.
Wajasiriamali  wakifanya  "  practical "  ya  kutengeneza  sabuni  ya  maji  kwa  vitendo  mara  baada  ya  kupokea  maelekezo  kutoka  kwa  waalimu  wa  ujasiriamali  kutoka  katika  Asasi  ya  RafikiElimu   Foundation. 
Mwalimu  wa  Ujasiriamali  kutoka  Taasisi  ya  RafikiElimu   Foundation, Mama  Hellen  Mbise  akielekeza  kwa  vitendo  namna  ya  kutengeneza  sabuni   za  maji. 
Mwalimu  Ashankira  Lupembe  akiwaonyesha  wanamfunzo  kitambaa  kilcho  fuliwa  kwa  kutumia   sabuni  aliyo  itengeneza  mwenyewe  wakati  wa  uzinduzi  wa  EUMIVI  PROJECT. 
Mwalimu  wa  Ujasiriamali  kutoka  Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation, Mama  Ashankira  Lupembe  akifua  kitambaa  kwa  kutumia  sabuni  iliyo  tengenezwa  wakati  wa  mafunzo  ya  utengenezaji  sabuni   ya  wakati  katika  uzinduzi  wa  mradi  wa  Elimu  ya  Ujasiriamali Mijini  &   Vijijini.
Mama  Ashankira  Lupembe, Mtaalamu  na  Mwalimu  wa  Ujasiriamali  kutoka  RafikiElimu  Foundation  akitoa  maelekezo  ya  namna  ya  kutengeneza  sabuni  ya  maji  kwa   vitendo. 
Mradi uliolenga  kupunguza  tatizo  la  ajira  nchini  kwa  kutroa  elimu  ya  ujasiriamali  kwa  maelfu  vijana  wa  kitanzania  waishio  mijini  na  vijijini  ifikapo  mwezi  Novemba  2014   umezinduliwa  rasmi  leo  jijini  Dar Es  salaam.  Uzinduzi  huo   ulio  fanyika  mapema  leo  katika  eneo  la  Shule  Ya  Msingi  Mlimani  iliyopo  katika  Chuo  Kikuu  Cha  Dar Es  salaam  na  kuhudhuriwa  na  makumi  ya  vijana  wa  kada  mbalimbali  jijini  Dar  es  salaam   uliambatana  na  mafunzo  ya  ujasiriamali   ambapo  wahudhuriaji  walipata  nafasi  ya  kujifunza  kutengeneza  sabuni  za  aina  mbalimbali  kutoka  kwa  wataalamu  wa   kutoka  katika  taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation, taasisi  inayo  jihusisha  na  maendeleo  ya  jamii.

Baadhi  ya  wajasiriamali  walio  hudhuria  katika   Uzinduzi  wa Mradi  wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini  uliofanyika   leo  jijini  Dar  Es  salaam. 
Akiulezea  mradi  huu,   mratibu  msaidizi  wa  mradi  huo   alisema   kuwa  mradi  huu  upo    katika  awamu  kuu  mbili.  Awamu  ya  kwanza   itafanyika  kuanzia  tarehe  01  Septemba  2012 hadi  tarehe  29 Septemba  2012, na  utafanyika  katika  mikoa   ya  Dar Es  salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Morogoro,  Dodoma  na Kilimanjaro, ambapo  mbali  na  kutoa  mafunzo  ya  ujasiriamali, asasi  itatafuta   vijana  kumi  na  wawili  kutoka  katika   hiyo  mikoa  saba   kwa  ajili   ya  kufanya  kazi  kama  wajitoleaji " volunteers"  katika  awamu  ya  pili  ya  mradi  itakayo  anza  rasmi  tarehe 01  Novemba  2012  na   kuchukua  miaka  miwili  hadi    Novemba  2014   ambapo  ndipo  itakapo  kuwa  tamati  ya  mradi  huu.

Awamu  ya  kwanza  ya  mradi  huu  inafanyika  katika  mikoa  ya  Dar  Es  salaam,  Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Dodoma, Mwanza  na  Mbeya.  Jijini  Dar  Es  salaam, mafunzo  yanafanyika  kwa  siku  tatu  kuanzia  tarehe 01  Septemba  2012  hadi  tarehe  04  Septemba  2012  katika  Shule  ya  Msingi  Mlimani  , iliyopo  katika  Chuo  Kikuu  Cha  Dar  Es  salaam...  Ratiba  kamili  ya  awamu  ya  kwanza  ya  mafunzo  haya  ni  kama  ifuatavyo :
1. ARUSHA, MOSHI  & MOROGORO :  Mafunzo  yatafanyika  kuanzia  tarehe  17 hadi  19 Septemba 2012..  Mwisho  wa  kujiandikisha  katika  " programme  hii " kwa  wakaazi  wa  ARUSHA, MOSHI  na  MOROGORO  ni  tarehe  15  Septemba  2012.
Baadhi  ya  wanafunzi  wa  ujasiriamali  waliohudhuria  katika  mafunzo  haya  wakifuatilia  darasa  kwa  makini. 
2. MWANZA, MBEYA   &  DODOMA :  Mafunzo  yatafanyika  kuanzia  tarehe  27 hadi  29 Septemba  2012.
Mwisho  wa  kujiandikisha  katika  programme  hii  kwa  wakaazi  wa  DODOMA, MBEYA  & MWANZA ni  tarehe  25  Septemba 2012.

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...