Skip to main content

ABG NORTH MARA YAGAWA MADAWATI 1,000 KWA SHULE ZA TARIME.


Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi zilizopo wilayani Tarime mkoa wa Mara wakifurahia msaada wa madawati zaidi ya 1,000 kutoka mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG).
Wanafunzi wa shule za msingi za serikali za wilaya ya Tarime, mkoa wa Mara, wakikaa sakafuni kabla ya kupata msaada wa madawati zaidi ya elfu moja kutoka mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG).
Msaada wa pikipiki tatu maarufu kama Bajaj ambazo mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) ulitoa kwa baadhi ya wananchi wa jamii zinazoishi karibu na mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara.
TARIME
Mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) umetoa msaada wa madawati zaidi ya 1,000 kwa shule za msingi zilizopo wilayani Tarime, mkoa wa Mara.
Msaada huo utakaoenda kwa shule 10 za msingi, utawanufaisha karibu wanafunzi 6,000 ambao kwa sasa wanalazimika kusoma wakiwa wameketi chini kwenye sakafu ya udongo.
Madawati hayo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 76.5 yametolewa na kampuni ya ABG kupitia mfuko wake wa maendeleo.
Shule zitakazofaidika na msaada wa madawati hayo ni Nyangoto, Marare, Nyamongo, Nyabhigena, Kerende, Genkuru, Bung’eng’e, Nyaisangero, Nyamwaga, Nyakunguru A na Nyakunguru B.
Shule hizo zina jumla ya wanafunzi wanaozidi 5,800, huku wanafunzi wengi wakiwa wanakaa sakafuni kutokana na kukumbwa na upungufu mkubwa wa madawati.
Akipokea msaada huo juzi, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele, aliishukuru kampuni ya ABG na mgodi wake wa North Mara kwa madawati hayo.
Henjewele alisema kuwa madawati hayo yatasaidia kuondoa kero ya muda mrefu ya shule hizo ya wanafunzi kukaa sakafuni na hivyo kusoma katika mazingira magumu.
“Hili ni tukio la kihistoria ambalo linaonesha jinsi mgodi na watu wanaoishi eneo hili walivyokuwa na mahusiano mazuri,” alisema.
Walimu pamoja na wanafunzi wa shule za Tarime walifurahia msaada huo na kusema kuwa utasaidia kuboresha mazingira ya elimu.
“Tunafuraha kubwa kukabidhi zaidi ya madawati 1,050 kwa shule zinazozunguka mgodi wa North Mara na hii inadhihirisha jinsi ambavyo jamii zinavyopata manufaa kutoka kwenye mgodi wetu,” alisema Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Gary Chapman.
Msaada huo wa madawati ulienda sambamba na kuzinduliwa kwa program ya Can Educate ambayo inatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye uwezo ambao wanatoka kwenye jamii maskini.
Mgodi huo pia ulitoa msaada wa pikipiki za Bajaj kwa wanakijiji watatu wenye ulemavu wa viungo.
Mgodi wa North Mara umekuwa ukitoa misaada mingi ya jamii zinazozunguka mgodi huo kwenye sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu na uwezeshaji wa kiuchumi.
Uongozi wa kampuni ya ABG pamoja na mgodi wa North Mara umekuwa ukifanya jitihafa kubwa kuboresha mahusiano na jamii zinazozunguka mgodi huo.
 
 
 


Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...