Skip to main content

Posts

NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU WA UJASIRIAMALI

Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation  inatangaza    nafasi  za  mafunzo  ya   UALIMU   WA   UJASIRIAMALI   kwa   waombaji   wenye   sifa   zifuatazo ; 1.    Mtanzania    mwenye  umri  wa  kuanzia  miaka  18  hadi  45. 2.Awe   na  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha   nne,  sita  na  kuendelea.  3. Aliye   na   utashi  na malengo  ya  kufanya kazi    kama  MWALIMU  WA  UJASIRIAMALI  kwenye  Mradi  Wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini. 4. Anayeweza    kuwasiliana   kwa    ufasaha   kwa   lugha   za   Kiswahili   na ...

TAARIFA FUPI YA UCHUNGUZI JUU YA MATUKIO YA MIMBA KWA WANAFUNZI WILAYA YA HANDENI, MKOANI TANGA

  Baadhi  ya  wanafunzi  wakihojiwa  na  mwandishi  wa  habari  hii( hayupo pichani  ) TAARIFA FUPI YA UCHUNGUZI JUU YA MATUKIO YA MIMBA KWA WANAFUNZI WILAYA YA HANDENI, MKOANI TANGA. UTANGULIZI Uchunguzi huu umefanyika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Uchunguzi umefanyika kuanzia Machi 19, 2013 katika Kata tatu za Wilaya ya Handeni, ambazo ni pamoja na Kata ya Chanika, Kata ya Vibaoni na Kata ya Kidereko. Uchunguzi huu wa kihabari ni mwendelezo wa utafiti uliofanyika Machi Mwaka jana (2012), kuangalia ukubwa wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia (GBV), katika vipengele vya Ubakaji, Watoto wa Kike Wanafunzi Kulazimishwa Kuolewa, Vitendo vya Ukeketaji, Vipigo kwa Wanawake pamoja na Vitendo vya Utelekezaji Watoto na Wanawake. Uchunguzi wa pili umefanyika kuangalia mrejesho wa matukio ya mimba na ndoa katika umri mdogo katika maeneo hayo, ikiwa ni mwaka mmoja tangu kufanyika kwa utafiti wa mwaka jana. MBINU ZA UCHUNGUZI...

NAFASI ZA MAFUNZO NA INTERNSHIP

                        NAFASI   ZA  MAFUNZO  NA  INTERNSHIP RafikiElimu   Foundation  ni   Taasisi   Isiyokuwa   ya   Kiserikali   ( NGO )  inayo   jihusisha   na   Maendeleo   Ya   Jamii nchini .  Taasisi   inatangaza   nafasi   za   mafunzo   ya   NGO  MANAGEMENT & OPERATION  kwa   vijana    wenye   sifa   zifuatazo : 1.         Umri   miaka   18  hadi 45. 2.       Elimu   kuanzia   kidato   cha  nne , sita na   kuendelea . 3.       Uwezo   wa   kuwasiliana   kwa   ufasaha   kwa   lugha   za   Kiswahili   na   kiing...

HII NDIO KUMBUKUMBU YA MIAKA 17 YA AJARI YA MELI YA MV BUKOBA ILIYOZAMA TAREHE 21 MAY

Meli ikiwa inazama na ikiwa imezungukwa na mitumbwi pamoja na boti ambazo zilisaidia kwenye uhokoaji   MV Bukoba ikiwa inazama ilikuwa ni tarehe 21 mei 1996    Makaburi ya Igoma ambako ndugu zetu waliokuwa wakisafiri kwa meli ya MV Bukoba walizikwa. RIPOTI ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv Bukoba, inasema usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37. Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.   Kila mwaka, ifikapo Mei 21, serikali inayosema haina dini, huongozana na viongozi wa madhehebu ya dini na waganga, kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.   Serikali ilishitaki aliyekuwa nahodha wa mv Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru, (sasa marehemu), Mkaguzi wa Mamlaka ya Ba...

NAFASI ZA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOROGORO.

                                NAFASI   ZA   MAFUNZO   YA   UJASIRIAMALI   MJINI  MOROGORO . RAFIKIeLIMU    MOROGORO    wanakuletea     SEMINA   YA   MAFUNZO   YA   UJASIRIAMALI . Mafunzo   yatakayo   fundishwa   ni   pamoja   na   Utengenezaji   wa   bidhaa   mbalimbali   kama   vile   ; Sabuni   za   aina   mbalimbali,   chaki, mishumaa, usindikaji,    utengenezaji   wa   manukato (   perfumes ), lotion, mafuta   ya   kujipaka, kiwi, mango   pickles, Chilly   Sauce, Tomato   Sauce    nakadhalika. WAPI  :  BERRICK EDUCATION CENTRE    karibu  na  SABASABA, mkabala na JENGO LA CCM MKOA MOROGORO. ...

UPDATE: WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MANZESE WAKUMBWA NA UGONJWA WA KUANGUKA

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu kutanda maeneo hayo. Tukio hilo limetokea kuanzia saa nne asubuhi ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha kushangaza waliendelea kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na kupigana kama vichaa. PICHA  KWA  HISANI  YA  BLOGS  MBALIMBALI.