Skip to main content

NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU WA UJASIRIAMALI





Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation  inatangaza    nafasi  za  mafunzo  ya  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI  kwa  waombaji  wenye  sifa  zifuatazo ;

1.    Mtanzania    mwenye  umri  wa  kuanzia  miaka  18  hadi  45.

2.Awe   na  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha   nne,  sita  na  kuendelea. 

3. Aliye   na   utashi  na malengo  ya  kufanya kazi    kama  MWALIMU  WA  UJASIRIAMALI  kwenye  Mradi  Wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini.

4. Anayeweza   kuwasiliana  kwa   ufasaha  kwa  lugha  za  Kiswahili  na  kiingereza.

5.  Awe  anaishi    katika   wilaya  ya  Ilala, Kinondoni  au  Temeke.



DHUMUNI   LA    MAFUNZO  HAYA
 Dhumuni  kuu  la  mafunzo  haya  ni  kuwaandaa  wahitimu  kufanya  kazi  kama  WAALIMU  WA  UJASIRIAMALI  katika  Mradi  Wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini  unaoratibiwa  na  Taasisi.  


 MUDA  WA  MAFUNZO  Mafunzo  haya  yatafanyika  kwa  muda  wa  mwezi  mmoja  kuanzia  tarehe  01 AGOSTU  2013..

BAADA  YA  KUHITIMU : Wahitimu  wa  mafunzo  haya, watapata  nafasi  ya   kufundisha  somo  la  Ujasiriamali    katika  vituo  vya  mafunzo  ya  ujasiriamali  katika  wilaya  mbalimbali  za  Tanzania  bara.
 ADA  YA  MAFUNZO: Ada  ya  mafunzo   haya ni  rahisi  sana.


FOMU  ZA  MAFUNZO : Fomu  za  mafunzo  haya  zinapatikana   kwa  SHILINGI  ELFU  KUMI  NA  MBILI ( Tshs. 12, 000/=)  tu  katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.

Mwisho  wa  kuchukua  fomu   za  kujiunga  na  mafunzo  haya  ni  tarehe  25  JULAI  2013.
Kwa  maelezo  zaidi  wasiliana  nasi  kwa  simu 0756606085 au 0782405936.

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...