Skip to main content

MAFUNZO YA KUTENGENEZA LOSHENI, MAFUTA YA KUJIPAKA NA PAFYUMU..

Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation, inapenda  kuwatangazia   vijana  wote  wa  kitanzania, nafasi  za   kushiriki  katika  mafunzo  ya  utengenezaji  wa  bidhaa  mbalimbali.  Bidhaa  zitakazo  fundishwa  ni  pamoja  na   UTENGENEZAJI  WA  MAFUTA  YA  KUJIPAKA, LOSHENI  na  MANUKATO.

SIFA  ZA  WASHIRIKI :  Mtu  Yoyote  anaweza  kushiriki  katika  mafunzo  haya.

ADA  YA  KUSHIRIKI  :  Ada  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  ni  Shilingi  ELFU  ISHIRINI  NA  TANO  TU ( Tshs. 25,000/= ).

Mafunzo  yatafanyika  kwa  muda  wa  siku  tatu  kuanzia  tarehe   01  AGOSTI  2013  hadi  tarehe  03  AGOSTI  2013. 

MAHALI  :  Mafunzo  haya  yatafanyika  katika  Chuo  kikuu  cha  Dar  Es  salaam.

Mwisho  wa  kujiandikisha  ni  tarehe  28  JULAI  2013.

WAHI  KUJIANDIKISHA  MAPEMA, KWANI  NAFASI  ZILIZOPO  NI  CHACHE.



 



Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...

SOMO LA TISA : USINDIKAJI WA MAZAO YA NAFAKA

Mahindi  yaliyo  toka  kuvunwa. 1 .   USINDIKAJI  WA   ZAO  LA  MAHINDI : Ili kuongeza matumizi ya mazao hayo na kudumisha ubora wake ni muhimu teknolojia za kusindika nafaka zitumike. Usindikaji pia huongeza thamani ya zao.                             KUSINDIKA MAHINDI Punje za mahindi hutumika kupika makande na husindikwa kupata unga unaotumika katika matumizi mbalimbali. Vile vile bidhaa nyingine zinazotokana na mahindi ni mafuta na wanga. KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA Kuna aina mbili za unga wa mahindi, unga wa mahindi yasiyokobolewa(Dona) na unga wa mahindi yaliyokobolewa (Sembe)  KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA WA DONA Vifaa • Mashine ya kukoboa • Mashine ya kusaga • Ungo • Debe • Mifuko • Chekeche ya nafaka Jinsi ya kusindika • Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche, ungo a...