Taasisi ya RafikiElimu Foundation inatangaza nafasi za mafunzo ya UALIMU WA UJASIRIAMALI kwa waombaji wenye sifa zifuatazo ;
1. Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45.
2.Awe na elimu ya kuanzia
kidato cha nne, sita na kuendelea.
3. Aliye na utashi na
malengo ya kufanya kazi kama MWALIMU
WA UJASIRIAMALI kwenye Mradi Wa Elimu
Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini.
4. Anayeweza kuwasiliana
kwa ufasaha kwa
lugha za Kiswahili na
kiingereza.
5. Awe
anaishi katika
wilaya ya Ilala, Kinondoni au
Temeke.
DHUMUNI LA MAFUNZO HAYA
Dhumuni kuu la mafunzo
haya ni kuwaandaa wahitimu kufanya kazi
kama WAALIMU WA UJASIRIAMALI katika Mradi
Wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini &
Vijijini unaoratibiwa na Taasisi.
MUDA WA MAFUNZO Mafunzo haya
yatafanyika kwa muda
wa mwezi mmoja
kuanzia tarehe 01 AGOSTU
2013..
BAADA YA KUHITIMU : Wahitimu wa mafunzo haya,
watapata nafasi ya kufundisha somo la
Ujasiriamali katika
vituo vya mafunzo
ya ujasiriamali katika
wilaya mbalimbali za
Tanzania bara.
ADA YA MAFUNZO:
Ada ya mafunzo haya ni SHILINGI ELFU SITINI NA TANO TU ( Tshs.65,000/=)
Mwisho wa
kuchukua fomu za
kujiunga na mafunzo
haya ni tarehe
25 JULAI 2013.
Comments
Post a Comment