Mradi wa Elimu
Ya Ujasiriamali Mijini
na Vijijini “ EUMIVI
PROJECT” ni mradi unao
ratibiwa na Taasisi
ya RafikiElimu Foundation
kwa kushirikiana na
mashirika rafiki. Mradi
huu ulizinduliwa rasmi
tarehe 01 Septemba
2012 jijini Dar
Es salaam na kuwahusisha
wajasiriamali wadogo wadogo
wa jijini Dar
Es salaam ambao
walipewa mafunzo ya
utengenezaji wa bidhaa
mbalimbali kama vile
sabuni za aina
zote, chaki na mishumaa
kwa kutaja vichache. Baada
ya hapo mafunzo
yalielekea katika jiji
la Arusha ambapo
wajasiriamali mbalimbali wa
jijini Arusha walipatiwa
mafunzo ya utengenezaji
wa bidhaa mbalimbali.
Mafunzo haya yalifanyika
pamoja utafiti uliokuwa ukifanywa
na taasisi hii
kuhusu changamoto mbalimbali
zinazo wahusu wajasiriamali wadogo
nchini Tanzania. Utafiti huo
wenye kichwa “ CHANGOMOTO
ZINAZOWAKABILI WAJASIRIAMALI WADOGO
WADOGO NCHINI TANZANIA” uligundua
mambo yafuatayo kama
changamoto hizo. Mambo hayo
ni pamoja na :
1. Ukosefu wa waalimu
wa Ujasiriamali :
Utafiti wetu umetuwezesha
kugundua kuwa Tanzania
ni miongoni mwa
nchi za Afrika
zinazo kabiliwa na
tatizo la ukosefu wa
waalimu wa kutosha wa
somo la ujasiriamali. Suala hili
lilitugharimu sana hata
sisi kama taasisi
katika awamu ya
kwanza ya mafunzo
ya mradi huu.
2. Ukosefu wa
Elimu Ya Uhakika
Ya Ujasiriamali: Hapa
ninazungumzia elimu ya
namna ya kufanya
ujasiriamali. Wajasiriamali
wengi wadogo wadogo
wa hapa Tanzania
hawana elimu ya
kutosha ya ujasiriamali, elimu inayo
weza kuwasaidia kufanya
ujasiriamali kwa mafanikio
makubwa. Hii inatokana
na ukosefu wa waalimu
wa ujasiriamali Tanzania.
3. Ukosefu wa
Elimu Uhakika Ya
Utengenezaji wa Bidhaa
Mbalimbali : Utafiti
wetu umegundua kuwa
wajasiriamali wengi wadogo wadogo wa
hapa Tanzania, hawana elimu
ya kutosha juu
ya utengenezaji na
uzalishaji wa bidhaa
mbalimbali kama vile
sabuni, mishumaa, chaki nakadhalika.. Endapo wajasiriamali
wakipewa ujuzi kuhusu
utengenezaji wa bidhaa
mbalimbali, ujuzi huo unaweza
kuwasaidia kuongeza wigo
wa shughuli zao
za kijasiriamali, kwa mfano
mjasiriamali ambaye alikuwa
hajui kutengeneza losheni, akipewa elimu
kuhusu utengenezaji wa
losheni maana yake atakuwa
na uwezo kujiongezea kipato
zaidi kupitia utengenezaji
wa losheni.
4. Kuwa na ujuzi
wa utengenezaji wa
bidhaa zinazo fanana : Kwa
mujibu wa utafiti
wetu, wajasiriamali wadogo wadogo
wa Tanzania wana
ujuzi wa utengenezaji
wa bidhaa zinazo
fanana. Bidhaa zinazo
tengenezwa na wajasiriamali
wengi wa Tanzania
ni sabuni za
maji, pamoja na mango pickle na Tomato Sauce
kwa kzitaja chache.
Hata hivyo, ujuzi huu
hauwasaidii sana wajasiraiamali hawa
kwa sababu karibu
kila mtu anaye
fanya ujasiriamali anafahamu
kuhusu utengenezaji wa
bidhaa hizo hizo
tu, so linapo kuja
suala la kuudha bidhaa
zao,jambo hili linasimama
kama changamoto.
5. Kutokuwa na
uwezo wa kutengeneza
bidhaa zenye ubora :
Utafiti wetu umetuwezesha
kugundua kuwa wajasiriamali wengi
wadogo wadogo wa
Tanzania, hawana uwezo wa
kutengeneza bidhaa zenye
ubora unaoweza kutoa
ushindani wa kibiashara
kwa wajasiriamali wa kati
na wakubwa ambao
nao pia wanajihusisha na
utengenezaji wa bidhaa
hizo hizo. Hali
hii imewafanya wajasiriamali wengi wadogo
wadogo wa Tanzania
kushindwa kuendeleza biashara
zao kwa sababu
ya kutengeneza bidhaa
zisizokuwa na kiwango
kinacho kidhi ushindani.
6. Kutokuwa na
sifa /uwezo wa kupata
mikopo kwenye taasisi
za kifedha : Wajasiriamali wengi
wadogo wadogo hapa nchini
Tanzania wana mawazo mazuri
ya kibiashara na
wengine wana elimu
ya msingi kuhusu
utengenezaji wa bidhaa mbalimbali
lakini wanashindwa kuyaweka
mawazo na ujuzi
wao katika vitendo
kwa sababu ya
kutokuwa na mitaji
ya kuanzisha biashara
na kwa wale
ambao tayari wamekwisha anza
biashara, wanashindwa kupata
pesa zaidi kwa
ajili ya kuendeleza
biashara zao. Moja kati
ya sababu zinazo
wafanya wajasiriamali wadogo
wadogo wa Tanzania
kushindwa kupata mikopo
kutoka katika taasisi
mbalimbali za kifedha
ni pamoja na
kutokukidhi sifa za
kukopeshwa lakini pili
kutokujua taratibu za
kuomba mikopo.
7. Kutokuwa na chombo
maalumu kw ajili
ya kutangaza shughuli
za wajasiriamali wadogo
wadogo wa Tanzania.
8. Kutofahamu sheria
na taratibu za
uanzishaji na uendelezaji
wa biashara na
kampuni.
9. Ukosefu wa
vifungashio vinavyo kidhi
matakwa ya bidhaa mbalimbali.
10. Ukosefu wa malighafi
za utengenezaji wa
bidhaa mbalimbali kama
vile sabuni, mishumaa, chaki,
losheni, mafuta ya kujipaka, pafyumu nakadhalika.
SULUHISHO LA CHANGAMOTO
ZINAZO WAKABILI WAJASIRIAMALI
WADOGO WADOGO WA
TANZANIA
Kufuatia changamoto hizo
hapo juu, Taasisi ya
RafikiElimu Foundation kwa
kushirikiana na mashirika
rafiki imeamua kufanya
mambo yafuatayo kwa
ajili ya kukabiliana na changamoto
hizo:
1. Kuanzisha mafunzo ya
Ualimu wa Ujasiriamali:
Taasisi ya
RafikiElimu imeamua kuanzisha
mafunzo ya UALIMU
WA UJASIRIAMALI kwa vijana
mbalimbali wa kitanzania. Mafunzo haya yatasaidia katika
kuwaandaa vijana mbalimbali
wa kitanzania kuwa
waalimu wa ujasiriamali
na hivyo kupunguza
tatizo la ukosefu
wa waalimu wa
ujasiriamali. Taasisi imepanga
kuwafundisha vijana wapato
mia moja ( 100)
katika kila wilaya
ya Tanzania bara
kama waalimu wa
ujasiriamali.
2. Kuanzisha MTANDAO
WA WAALIMU WA
UJASIRIAMALI TANZANIA : Mtandao
huu utawahusisha vijana
walio hitimu mafunzo
ya ualimu wa
ujasiriamali, na utafanya kazi
na kuwa na
ofisi katika wilaya
zote za Tanzania
bara. Mtandao utahusika na
kuratibu shughuli zote
za mradi katika
wilaya husika kama
vile kusimamia utolewaji
wa mafunzo ya
ujasiriamali .
3. Kuanzisha vituo vya
mafunzo ya ujasiriamali
katika wilaya zote
za Tanzania bara. Vituo hivi vitahusika
na kutoa mafunzo
ya ujasiriamali kwa wajasiriamali wadogo
wadogo kwenye wilaya
zote za Tanzania
bara. Vituo hivi vitasimamiwa
na ofisi ya
mtandao wa waalimu
wa ujasiriamali katika
wilaya husika.
4. Kuanzisha vikundi
vya kuweka na
kukopa “SACCOSS” pamoja na VICOBA katika
wilaya zote za
Tanzania bara.Vikundi hivi
vitawahusisha waalimu wa
ujasiriamali pamoja na
wajasiriamali wadogo wadogo
watakao jiunga na
mafunzo yetu na
vitafanya kazi katika
malengo ya kuwa
benki ya kijamii “ Community Bank “
5. Kuanzisha jarida
maalumu litakalo husika
na kutangaza bidhaa
na shughuli za
wajasiriamali wadogo wadogo waliopitia
mafunzo yetu. Jarida hilo
litaitwa “ MJASIRIAMALI” na litasambazwa
katika wilaya zote
za Tanzania bara. Jarida
hili litawasaidia sana
wajasiriamali wadogo wadogo kutangaza
biashara zao.
6. Kuanzisha maonyesho
madogo madogo ya
biashara yatakayo husu
bidhaa za wajasiriamali
wadogo wadogo wa
Tanzania bara.
7. Kuanzisha mashindano na tuzo mbalimbali
yatakayo wahusisha wajasiriamali
wadogo wadogo wa Tanzania
bara. Mfano: mashindano ya kushindanisha
ubora wa bidhaa
za wajasiriamali wadogo
wadogo. Tuzo hizi zitachangia
katika kuzitangaza bidhaa
za wajasiriamali husika lakini
pia zitasaidia katika kuongeza ari
na ufanisi kwa
wajasiriamali wadogo wadogo
wa Tanzania bara.
8. Kushirikiana na
wajasiriamali wa nje
ya Tanzania kufanya
maonyesho ya wajasiriamali
wadogo wadogo ili
kusaidia kuzitangaza biashara
na shuguli za wajasiriamali
wadogo wadogo wa
Tanzania bara.
9. Kuanzisha duka
la kuuza malighafi
zinazo tumika katika
kutengeneza bidhaa mbalimbali
kama vile mafuta
ya kujipaka, losheni na
pafyumu. Malighafi hizo zitauzwa
kwa bei nafuu
na zitasambazwa katika
wilaya zote za
Tanzania bara.
10. Kuanzisha duka
la kuuza vifungashio
kwa wajasiriamali wadogo
wadogo wa Tanzania
bara.
11. Lengo la
Mradi :
Lengo la mradi
huu ni kuwatrain
walimu wa ujasiriamali
wapatao mia moja
katika kila wilaya
ya Tanzania Bara na
kisha kuwatumia kuunda
MTANDAO WA WAALIMU
WA UJASIRIAMALI TANZANIA, utakao
husika na kutoa
mafunzo ya ujasiriamali
kwa wajasiriamali wadogo
wadogo waliopo katika
wilaya wanazo ishi .
MAFUNZO YATAKAYO
TOLEWA :
Mafunzo yatakayo
tolewa kwa
wanafunzi wa ualimu wa
ujasiriamali katika mradi
huu ni pamoja
na utengenezaji & uzalishaji wa
bidhaa mbalimbali kama
vile sabuni, mishumaa, chaki,
maji ya betri, manukato ( perfume ),
losheni, mafuta ya kujipaka, usindikaji wa
vyakula, usindikaji wa bidhaa
za ngozi kama
vile viatu, mikanda na
mabegi. Uanzishaji &
uendelezaji wa taasisi zisizokuwa
za kiserikali ( NGO Management & Operation ),uanzishaji
wa kampuni za
kibiashara, uanzishaji wa SACCOSS na
VICOBA nakadhalika.
UTARATIBU WA MAFUNZO KWA WAALIMU
WA UJASIRIAMALI
Mafunzo haya yatatolewa
kwa awamu mbili, awamu ya kwanza
itakuwa ni kwa wakaazi wa
Dar Es salaam, ambayo itaanza
tarehe 01 Agosti 2013 hadi
tarehe 20 Agosti 2013, na
awamu ya pili
ya mafunzo itaanza
tarehe 01 Septemba 2013
hadi tarehe 20 Septemba
2013 na yata
wahusisha wakaazi wa
mikoa mingine iliyo
baki.
MAFUNZO YA DAR ES SALAAM.
Mafunzo ya Dar Es
salaam yataanza tarehe 01
AGOSTI 2013 na yatafanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam , ( SEHEMU YA MLIMANI )
MAFUNZO YA NJE YA DAR ES
SALAAM.
Mafunzo yatakayo fanyika
nje ya mkoa
wa Dar Es
slaam yatafanyika kuanzia tarehe 01 SEPTEMBA ambapo wanafunzi wa ualimu wa ujasiriamali watakao hitimu katika mafunzo ya Dar Es salaam, watatembelea wilaya tofauti tofauti za Tanzania bara kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi wa mafunzo haya waliopo mikoani.
BAADA YA KUHITIMU
MAFUNZO
Baada ya kuhitimu
mafunzo haya wahitimu
wote wataunda mtandao
wa waalimu wa
ujasiriamali nchini Tanzania
ambao utafanya kazi
katika wilaya zote
za Tanzania bara. Mtandao
utahusika na kuanzisha
vituo vya ujasiriamali
katika wilaya zote
za Tanzania bara. Vituo
hivi vitahusika na
kutoa mafunzo ya
ujasiriamali kwa bei
nafuu kwa wajasiriamali
wadogo wadogo waliopo
katika wilaya husika.
Hii ni nafasi
nzuri kwa vijana
wa kitanzania wasio
kuwa na ajira, kuweza
kujiajiri kupitia mradi huu.
ADA
YA MAFUNZO:
Ada ya mafunzo
haya ni Shilingi
Elfu Sitini na
Tano tu za
Kitanzania ( Tshs.65,000/=).
FOMU
ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO
HAYA : Fomu
za kujiunga na
mafunzo haya zinapatikana
kwa shilingi Elfu Kumi
na Mbili Tu ( Tshs.12,000/=) katika
ofisi zetu zilizopo
katika eneo la CHANGANYIKENI karibu
na Chuo Cha
Takwimu.
Mwisho
wa kuchukua fomu
za kujiunga na
Mafunzo Haya: Mwisho wa
kuchukua fomu za
kujiunga na mafunzo
haya ni tarehe
25 Julai 2013. Mafunzo
yataanza tarehe 01
AGOSTI 2013.
Comments
Post a Comment