NAFASI ZA MAFUNZO NA INTERNSHIP
RafikiElimu Foundation ni Taasisi Isiyokuwa ya Kiserikali ( NGO ) inayo jihusisha na Maendeleo Ya Jamii nchini. Taasisi inatangaza nafasi za mafunzo ya NGO MANAGEMENT & OPERATION kwa vijana wenye sifa zifuatazo :
1. Umri miaka 18 hadi 45.
2. Elimu kuanzia kidato cha nne, sita na kuendelea.
3. Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha za Kiswahili na kiingereza.
4. Uwezo wa kusoma na kuelewa mwenyewe kwa njia ya masafa.
5. Uwe mkaazi katika mojawapo kati ya wilaya zilizopo Tanzania bara.
Mafunzo haya yatatolewa kwa njia ya posta na yatatolewa kwa miezi mitatu. Mwezi mmoja ni wa mafunzo kwa nadharia na miezi miwili ni ya mafunzo kwa vitendo ambayo yatafanyika katika taasisi zisizokuwa za kiserikali.
WASHIRIKI WOTE WA MAFUNZO WATAPEWA NAFASI YA KUFANYA INTERNSHIP KATIKA TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI
( NGOs ) KWA MUDA WA MIEZI MIWILI.
Mafunzo yataanza tarehe 01 JULAI 2013.
FOMU ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO:
KWA WAKAAZI WA DAR ES SALAAM.
Kwa wakaazi wa Dar Es salaam , fomu za kujiunga na mafunzo haya zinapatikana katika maeneo yafuatayo :
1. Katika ofisi zetu zilizopo katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU.
2. Katika Ofisi Kuu za POSTA zilizopo MJINI KATI.
BEI YA FOMU YA MAOMBI NI SHILINGI ELFU KUMI NA MBILI TU ( Tshs. 12,000/=)
KWA WAOMBAJI WA MIKOANI.
Kwa waombaji wa mikoani watume maombi ya kutumiwa fomu za kujiunga na mafunzo haya kupitia barua pepe yetu ambayo ni: rafikielimutanzania@gmail.com
Mwisho wa kuchukua fomu za maombi ni tarehe 25 JUNI 2013.
Na Mwisho wa kuomba kutumiwa fomu za maombi ni tarehe 25 JUNI 2013.
ADA YA MAFUNZO HAYA NI NAFUU SANA.
Comments
Post a Comment