|
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Rafiki Elimu Foundation, Bwana Omary Baraka Mbwetom ( wa mwisho waliosimama ) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na mwalimu wa Shule Ya Sekondari Ya Kisaza iliyopo Wilayani Handeni Mkoani Tanga. |
|
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pangambili iliyopo wilayani Handeni mkoani Tanga wakilima. |
|
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pangambili iliyopo wilayani Handeni mkoani Tanga. |
|
|
Wanafunzi wa Shule ya Kwaludege Sekondari wakichota maji bwawani kwa ajili ya matumizi mbalimbali. |
|
Wanafunzi wa Shule Ya Sekondari Kisaza, iliyipo wilayani Handeni mkoani Tanga. |
|
Kabuku Secondary School, Handeni, Tanga. |
|
Wanafunzi wa Kabuku Sekondari School, iliyipo wilayani Handeni mkoani Tanga. |
|
|
Shule ya Sekondari Kwaludege iliyopo wilayani Korogwe, mkoani Tanga. |
|
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kwaludege wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Rafiki Elimu Foundation pamoja na walimu wa shule hiyo. |
Wanafunzi yatima wa kike na wanaoishi katika mazingira magumu wapatao mia moja kumi na watano
( 115 ) wanao soma katika shule za sekondari za
Kwaludege Secondary School, Pangambili Secondary School, Kabuku Secondary School pamoja na
Kisaza Secondary School zilizopo katika wilaya za Handeni na Korogwe Mkoani Tanga. wamefanikiwa kupata udhamini wa kusomeshwa kwa kulipiwa ada ya shule pamoja na vifaa vinginevyo muhimu katika masomo kama vile vitabu vya ziada na kiada.
Udhamini huo, umetolewa na Asasi Isiyokuwa ya Kiserikali iitwayo "
Rafiki Elimu Foundation " ya jijini Da Es salaam kupitia mradi wake "
Elimisha Msichana Project " uliolenga katika kutoa msaada wa kuwasomesha wanafunzi wa kike wanao soma katika shule za sekondari zilizopo maeneo ya vijijini na ambao wanaishi katika mazingira magumu( mfano watoto yatima, na wale wenye wazazi wazee ama walemavu ) kwa kuwalipia ada pamoja na kuwapatia vifaa vingine muhimu katika masomo kama vile vitabu vya ziada na kiada. Walengwa wakuu katika mradi huu ni wanafunzi wa kike katika shule za sekondari zilizopo maeneo ya vijijini na ambao wanaishi katika mazingira magumu, mfano yatima, wenye wazazi wazee sana na walemavu.
Akiongea na waandishi mbalimbali wa habari, Katibu Mkuu wa Taasisi ya
Rafiki Elimu Foundation, Bwana,
Omary Baraka Mbweto, amesema yakuwa , lengo la mradi ni kuhakikisha wanawasaidia wasichana elfu tano wanaosoma katika shule za sekondari zilizopo vijini na wanaoishi katika mazingira magumu katika mikoa yote ya Tanzania Bara, ambapo kwa kuanza taasisi yake imeanza na kuwalipia ada za masomo pamoja na vifaa mbalimbali vya shule wanafunzi wapatao mia moja na kumi na tano katika wilaya ya Handeni ambayo ipo katika mkoa wa Tanga.
|
Katibu Mkuu wa Rafiki Elimu Foundation ( Wa Pili kutoka kulia, waliosimama ) akiwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kwaludege, iliyopo Handeni, Mkoani Tanga ambao wanafadhiliwa na Taasisi ya Rafiki Elimu Foundation. Wa kwanza kulia ( waliosimama/aliye vaa shati la buluu ) ni Mwalimu katika shule hiyo ya sekondari. |
" Mradi huu, hautaishia hapahapa Handeni, Tanga bali utakuwa ni mradi wa nchi nzima, baada ya hapa tutaelekea wilayani Manyara ambapo tunaenda kufanya utafiti katika wilaya ya Babati na kutoa msaada wetu huo, kabla ya kuelekea katika wilaya za Kondoa ( Dodoma ) Arumeru ( Arusha ). Mkuranga, Rufiji, Kisarawe na Mafia ( Pwani ). Alisema Ndugu Mbweto.
" Tukimalizana na wilaya hizo tutaelekea katika wilaya nyinginezo za Tanzania Bara " aliongeza.
Bwana Omary Mbweto alisema kuwa, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanao saidiwa katika mradi huu ni wale wenye uhitaji kweli, yani yatima, watoto wenye wazazi wazee sana ama walemavu, taasisi yake imekuwa makini mno kwa kuhakikisha kuwa nyaraka zote muhimu zinazo thibitisha kuwa mwanafunzi husika ni yatima na ama ana ishi katika mazingira magumu.
Mradi wa
Elimisha Msichana Project mbali na kuwalipia ada na mahitaji muhimu ya shuleni kama vile vitabu na kiada na ziada wanafunzi wa kike yatima wanaoishi katika mazingira magumu waliopo katika shule za sekondari zilizopo katika maeneo ya vijijini nchini Tanzania, pia umelenga kutoa elimu kwa watanzania wote kuwahasisha kujenga utamaduni wa kuwasomesha watoto wa kike, na yatima wanaoishi katika mazingira magumu.
Mbali na kujihusisha na maendeleo ya elimu nchini Tanzania, taasisi ya Rafiki Elimu Foundation inahusika na kutoa msaada wa kisheria kwa watu mbalimbali wenye matatizo ya kisheria lakini hawana uwezo wa kumudu gharama za mawakili, huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wanawake, walemavu, wazee na katika masuala ya elimu.
To me i would like to join this RafikiElimu Foundation programs but i search for the table of registration process in mwanza but there is a list of starting class period in mwanza and morogoro.So please i would like to know the time of registration in mwanza for those not yet registed.Because i am the among not yet registed but i would like to be among the students in that program.And me I'm from mwanza -Tanzania.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeletehabari naitwa simon dominick, natafuta mfadhili wa kunisomesha kwa sasa nasoma chuo cha biashara cbe, wazazi wangu hawana uwezo wa kunisomesha, kama kuna msamaria mwema naomba anisaidie
ReplyDelete0717697657
simondominick@yahoo.com
Grace Nursery school seeks your support in establish a better system for learning and to help raise young leaders of tomorrow to realise their future dream and grow spiritually.
ReplyDeleteThe school is based in Mbeya Tanzania and it's under only 3 teachers,your support is really needed in improving the istitution.
your support in any way will be greatly appreciated.
for more information:
Phone number:+254721452113
+255754749035
Email address:hb2samweli@yahoo.com
hb2samweli@gmail.com
Fb account:Grace nursery & primary school
your support is very important, keep supporting these vulnerable ones
ReplyDelete