|
Juu wanafunzi wa shule za msingi Ipembe, Nyerere, na Unyankindi zilizopo katika manispaa ya Singida wakiwa katika maandamano.
|
|
Mwanafunzi akiwa anawafndisha wanafunzi wenzake baada ya walimu kugoma. Hii imetokea huko mkoani Mbeya siku ya jana tarehe 30 Julai 2012. Picha kwa hisani ya MJENGWA BLOG. |
Mgomo uiso na kikomo ulio andaliwa na Chama Cha Waalimu Tanzania ( CWT ) ambao umeanza rasmi siku ya tarehe 30 Julai 2012 kwa muda usiojulikana hadi hapo serikali itakapo sikiliza matakwa ya waalimu, umekuwa na athari kubwa sana kwa wanafunzi. Waathirika wakuu wa mgomo huu ni wanafunzi ambao wanajiandaa na mitihani ya taifa ambayo inakaribia kuanza kufanyika nchi nzima , mfano darasa la saba nakadhalika. Sisi kama RafikiElimu Foundation tunaiomba serikali imalize mgogoro huu haraka iwezekanavyo ili watoto wetu waweze kuendelea na masomo yao kama kawaida. Mungu Ibarika Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Comments
Post a Comment