Taasisi ya RafikiElimu Education Consultancy, kupitia Mradi wa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa njia ya videon( VIDEO - MAFUNZO PROJECT) inakutangazia wewe kijana wa ki Tanzania, nafasi ya kujiunga na mafunzo ya Ujasiriamali kwa njia ya video. Masomo yatakayo fundishwa ni pamoja na 👇 1. Jinsi ya kutengeneza pipi za kihindi ( Pipi za Kihindi) ni pipi zinazo tengenezwa Nyumbani kwa kutumia sukari ya kawaida ama sukari guru. Pipi hizi ni pipi zinazo pendwa Sana na watoto wa shule za msingi na sekondari. Kijana akijua jinsi ya kutengeneza pipi hizi, anakuwa amepata ujuzi utakao muwezesha kujitengenezea kipato chake halali kupitia kutengeneza pipi hizo za kihindi na kwenda kuziuza mashuleni 2. Jinsi ya kutengeneza mashine za kutotolea vifaranga wa kuku ( Incubators) 3. Jinsi ya kutengeneza chaki. 4. Jinsi ya kutengeneza sabuni za aina mbalimbali. 5. Jinsi ya kutengeneza ice cream, na juice za aina mbalimbali. 6. Pamoja na masomo mengine mengi....