Amina Mwamkinga alisema tangu tarehe
tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni
hapo wakimtuhumu kuwa mchawi majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba
hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi hali
iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za
kujisitiri kama Shuka nk.
Hapa Amina akimsimulia mkasa mzima mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango mara baada ya kupata maelezo yote ya Amina mwandishi wetu alimpigia simu katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mbeya afike ofisi ya Mbeya yetu ili wasaidiane kutatua tatizo hilo.
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alifika ofisi ya Mbeya yetu na kuanza kumsikiliza Amina.
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale akiwa makini kumsikiliza Amina katika ofisi ya Mbeya yetu
========= ======== ============
KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari
Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule
Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa
anajihusisha na imani za Kishirikina.
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20)
ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa
Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo
kupata taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni
Mshirikina.
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru
mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua
ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo
akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa
alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo
majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi
aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na
baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.
Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule
hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo
baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu
yake.
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun iliyoko
Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa
uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili
aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne
Mwakani.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya,
alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba
walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa
wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili
ahamie.
Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale
alisema alikuwa halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko
nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa
Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa
taarifa kwenye shirika linalolipa.
Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under
the Samesun Omary Mfaume amesema kwamba hana taarifa zozote kuhusiana
na tukio hilo na kuongeza kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa
moja ili umweleze juu ya kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule
nyingine zifanyika haraka ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama
kawaida.
CREDIT: MBEYA YETU BLOG.
KUTOKA RAFIKIELIMU BLOG : Tunalaani vikali sana kitendo kilicho fanywa na uongozi wa shule ya sekondari Hollywood kumfukuza shule binti huyu mlemavu kwa tuhuma ambazo chanzo chake ni imani potofu, tunampa pole binti huyu na tunawaomba wanao husika na mamlaka kuingilia kati suala hili ili kumsaidia binti huyu aweze kuendelea na masomo yake. Tunamuomba Mungu ampe moyo wa subira binti huyu katika kipindi kigumu hiki anacho pitia katika maisha yake.
Comments
Post a Comment