NAFASI ZA KAZI ( FOOD PRODUCTION ) RafikiElimu Education Consultancy ni Taasisi inayo jihusisha na usimamizi wa maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wanao soma katika shule za msingi na sekondari nchini Tanzania, pamoja na mafunzo ya ujasiriamali. Taasisi Kwa kushirikiana na shule mbalimbali za msingi na sekondari katika mikoa ya Dar Es Salaam na Mtwara inaratibu mradi wa “ MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA PIPI ZA VIJITI” almaarufu kama “ PIPI ZA KIHINDI”, kwa vijana waliomaliza kidato cha nne. Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea vijana hao , uwezo wa kujiajiri wenyewe kwa kutengeneza na kuuza pipi hizo kwenye shule za msingi na sekondari ambazo zinashirikiana na taasisi katika mradi huu. Kupitia mradi huu, taasisi inatangaza nafasi za kazi ya kufundisha namna ya kuandaa na kutayarisha pipi za vijiti ( Pipi za kihindi ). Mafunzo haya yatatolewa kwa vijana wanao simamiwa na taasisi yetu katika mradi huu. SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI : 1.
NAFASI ZA KAZI MTAFITI MSAIDIZI : NAFASI KUMI NA MBILI ( ATHARI ZA MIMBA ZA UTOTONI, ENEO LA MZINGATIO, LINDI & MTWARA) RafikiElimu Education Consultancy ni Taasisi binafsi inayo jihusisha na usimamizi wa maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wanao soma QT pamoja na wale wanao jiandaa kurudia mitihani ya sekondari ( Re-seaters). Taasisi ina andaa kitabu pamoja na documentary maalumu kuhusu ATHARI ZA MIMBA ZA UTOTONI katika wilaya mbalimbali zilizopo katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Kupitia project hii, Taasisi inatangaza nafasi kumi na mbili za kazi ya “ Mtafiti Msaidizi” atakae msaidia mwandishi mkuu wa kitabu hiki kupata taarifa muhimu zitakazo muwezesha kukamilisha zoezi la kuandika kitabu hiki. MAJUKUMU YA KAZI HII : ni pamoja na kuwatafuta wahanga wakuu wa tatizo la mimba za utotoni yani wasichana waliopata mimba utotoni na kuharibiwa ndoto zao za kuendelea na masomo yao kwa ajili ya kufanya mahojiano na mwandishi mkuu wa kitabu hiki. SIFA ZA MWOMBAJI : 1.