Ukifika nje ya geti la Kituo cha Masanga tangu mwezi huu wa 12 ulipoanza utakutana na huu ujumbe ''HAKATWI MTU HAPA'' hiki ni kituo cha kuzuia ukeketaji (TFGM) ambacho kinatoa mafunzo ya ukeketaji mbadala na tohara salama... kwa sasa kuna watoto zaidi ya 600 ambao wamekimbilia hapa ili wasikeketwe tangu msimu huu ulipoanza mwezi wa 12/2014...
Mwezi wa 12 ni mwezi wa kufanya tohara mkoani Mara ambapo watoto wengi huwa wamefunga shule na hivyo kupelekea watoto wa kike hukeketwa...
Mabango haya yamebeba ujumbe tofautitofauti kwa lengo la kuifikishia jamii kilio chao kutokana na hii mila yao ya Ukeketaji...
Nimeona ni busara kuwaomba Umma tushirikiane kuwasaidia watoto hawa hasa kipindi hiki kigumu ambacho wamekimbia kukeketwa wakingojea msimu uishe mwezi huu wa 12 warudi makwao wakaendelee na shule... yaani hawana hata maji! kama ujuavyo maji ni muhimu sana kwa binadamu, na huwa wanategemea maji ya mvua!!! sasa mvua hazijanyesha hivi karibuni... pia hawana chakula, pedi, nguo, viatu, kama una maswali zaidi unaweza kumuuliza mkuu wa kituo hicho Sister Germana... Lakini chondechonde nakuomba tuwasaidie wako kwenye hali mbaya...
Habari hii nimeitoa www.wanawakelivetv.com
Mahindi ni miongoni mwa mazao ya chakula ambayo unga wake unatumika kutengeneza unga lishe. UNGA LISHE : Ni unga bora na unao hitajika sana katika kuborehs afya za watoto, wazee na wagonjwa. Ukiwa kama mjasiriamali mdogo, ni muhimu kujua namna ya kutengeneza unga lishe, kwani malighafi zinazo tumika katika utayarishaji wa unga huu zinapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu, hivyo basi hata kwa wewe mwenye mtaji mdogo, unaweza kufanya biashara hii bila ya kuhitajika kuwa na mtaji mkubwa jambo linalo chukuliwa...
Comments
Post a Comment