Wanafunzi wa shule ya sekondari. |
Jumla
ya wanafunzi 438,960 kati ya wanafunzi 451,392 waliofaulu mtihani wa
darasa la saba nchini Tanzania wamechaguliwa kujiunga na kidato cha
kwanza katika shule za serikali za sekondari kwa awamu ya kwanza.
Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa
Akitangaza
matokeo ya ufaulu huo kwa vyombo vya habari na wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga kidato cha kwanza, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu
Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia
97.23 ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo.
Naibu waziri, Majaliwa amesema kati ya wanafunzi waliochaguliwa
wasichana ni 219,996 sawa na asilimia 97.1 na wavulana 218964 sawa na
asilimia 97.28 na kuongeza kuwa takwimu hizo zinaonesha kuwa idadi ya
wanafunzi waliochaguliwa imeongezeka kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na
96.3 ya waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka 2013.
Waziri Majaliwa ametoa wito kwa halmashauri kwa kushirikiana na wadau
wote wa Elimu kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea
wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha Kwanza mwaka 2015.
Pia amewahimiza wazazi, walezi, na jamii kushirikiana na uongozi wa
wilaya, halmashauri, na shule kuhakikisha kwamba wanafunzi wote
waliochaguliwa wanaandikishwa, na kuhudhuria hadi watakapomaliza elimu
ya sekondari.
Halmashauri zilizobakiza wanafunzi 12,432 katika awamu ya Kwanza ni
Dodoma, (9824) Dar es salaam (1414), Morogogoro (752), Mtwara (281) na
Katavi (161) .
Waziri Majaliwa ameziagiza Halmashauri hizo kukamilisha ujenzi wa
vyumba vya madarasa ili kuwawezesha wanafunzi hao kujiunga na Kidato cha
Kwanza ifikapo mwezi Machi.
CREDIT : VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI.
Comments
Post a Comment