Skip to main content

NAFASI ZA KAZI ( WASAIDIZI WA KAZI ZA OFISINI/ OFFICE MESSENGERS/ MESENJA WA OFISINI)

 





NAFASI  ZA  KAZI

( WASAIDIZI WA KAZI ZA OFISINI/ OFFICE MESSENGERS/MESENJA WA OFISINI)


RafikiElimu Education Consultancy ni  Taasisi inayo jihusisha na usimamizi wa maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wanao soma QT ( Qualifying Test) pamoja na wale wanao jiandaa kurudia mitihani yao ya sekondari ( Re-seaters).

Taasisi inaratibu na kusimamia program maalumu ya kuwasaidia  wahitimu walio feli kidato cha nne, kupata nafasi za kazi ya UMESENJA WA  OFISINI kwenye ofisi mbalimbali ili waweze kupata kipato  kitakacho wasaidia kujiendeleza kitaaluma  kupitia taasisi yetu.

 

Majukumu ya kazi hii ni pamoja na : kufanya usafi wa ofisi , kupika chakula cha wafanyakazi,kufua nguo za wafanyakazi, kupokea wageni wa ofisi, kutumwa kazi mbalimbali za ofisi ndani na nje ya ofisi, nakadhalika.  

 

SIFA ZA MWOMBAJI

1. Awe wa jinsia  yoyote ( yani wa kike au wa kiume)

2.  Awe muhitimu alie feli kidato cha nne kwa kupata Division Zero au Four  mwenye nia ya dhati ya kurudia mitihani yake ya kidato cha nne.

 3.  Awe amemaliza kidato cha nne kati ya mwaka  2023  hadi 2022 ( isiwe chini ya hapo)   na

4. Awe tayari kuanza kazi mara moja katika ofisi yoyote ambayo atapangiwa na taasisi.  

 

Tuma maombi yako  kupitia barua pepe ( email ) yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.com .

  Maombi yako yaambatanishwa na passport size zako mbili za rangi ulizo piga hivi karibuni.  Katika maombi yako taja mwaka ulio maliza shule na mahali unapoishi.  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe  15 APRILI  2024.  Kwa maelezo zaidi, endelea kututembelea kila kitu  kupitia tovuti yetu :

www.rafikielimu.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...