NAFASI ZA KAZI
MTAFITI MSAIDIZI :
NAFASI KUMI NA MBILI
( ATHARI ZA
MIMBA ZA UTOTONI, ENEO LA MZINGATIO, LINDI & MTWARA)
RafikiElimu Education Consultancy ni Taasisi binafsi inayo jihusisha na usimamizi wa maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wanao soma QT pamoja na wale wanao jiandaa kurudia mitihani ya sekondari ( Re-seaters).
Taasisi ina andaa kitabu pamoja na documentary maalumu kuhusu ATHARI ZA MIMBA ZA UTOTONI katika wilaya mbalimbali zilizopo katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Kupitia project hii, Taasisi inatangaza nafasi kumi na mbili za kazi ya “ Mtafiti Msaidizi” atakae msaidia mwandishi mkuu wa kitabu hiki kupata taarifa muhimu zitakazo muwezesha kukamilisha zoezi la kuandika kitabu hiki.
MAJUKUMU YA KAZI HII : ni pamoja na kuwatafuta wahanga wakuu wa tatizo la mimba za utotoni yani wasichana waliopata mimba utotoni na kuharibiwa ndoto zao za kuendelea na masomo yao kwa ajili ya kufanya mahojiano na mwandishi mkuu wa kitabu hiki.
SIFA ZA MWOMBAJI :
1. Awe wa jinsia ya kike mwenye elimu ya kuanzia kidato cha nne na mwenye taarifa za kutosha kuhusu wahanga wa tatizo la mimba za utotoni.
2. Awe mwenyeji wa Lindi au Mtwara anaeishi Lindi au Mtwara, kwa sababu project hii itafanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
3. Awe na bidii ya kazi , nidhamu na mwenye kujituma.
Tuma maombi yako kupitia barua pepe ( e.mail) yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.com .
Mwisho wa
kupokea maombi ni tarehe 15 APRILI 2024.
Kwa maelezo zaidi,
tutembelee kupitia tovuti yetu :
Comments
Post a Comment