Taasisi ya
RafikiElimu Foundation kupitia
Mradi wa Elimu
Ya Ujasiriamali Mijini
na Vijijini ( EUMIVI
-Project ) imejipanga kutoa
mafunzo ya UALIMU
WA UJASIRIAMALI kwa
vijana wapatao watano
kutoka katika kila
kata ya jiji
la Dar Es
salaam.
Mafunzo haya
yataanza rasmi siku
ya tarehe 02
Machi 2014 saa
tano kamili asubuhi
katika ukumbi wa
Chuo Cha RAFIKIELIMU
COLLEGE uliopo katika
eneo la CHANGANYIKENI
karibu na CHUO
CHA TAKWIMU.
Akizungumza na
RafikiElimu BLOG, Mratibu Msaidizi
wa Mradi wa
Elimu Ya Ujasiriamali
Mijini & Vijijini
kanda ya Dar
Es salaam, Ndugu ARISTARICK
MALLYA amesema kuwa, lengo
la mafunzo hayo
ni kuwajengea vijana
hao uwezo wa
kutoa mafunzo ya
ujasiriamali kwa vijana
wenzao waliopo katika
kata wanazo ishi.
Awamu
ya kwanza ya
Mradi huu ilianza
mnamo tarehe 01
Septemba 2012 ambapo
sisi kama taasisi
kwa kuwatumia wataalamu
wachache tulio nao,
tulizunguka katika wilaya
mbalimbali nchini Tanzania
kwa ajili ya
kutoa mafunzo haya.
Moja kati
ya changamoto tulizo
kutana nazo, ni uhaba
wa waalimu wa
ujasiriamali nchini Tanzania.
Sekta ya
ELIMU YA UJASIRIAMALI nchini Tanzania, inakabaliwa na
changamoto ya UHABA
WA WAALIMU WA
UJASIRIAMALI.
Hii ni
changamoto kubwa sana
ambayo inahitaji ufumbuzi
wa haraka ili
kuwasaidia wajasiriamali wadogo
wadogo waliopo katika
maeneo ya mijini
na vijijini.
Kwa kuanza
tutaanza kutoa mafunzo
kwa vijana kumi (
10 ) kutoka katika
kila kata ya
mkoa wa Dar
Es salaam.
Baada ya
mafunzo haya, vijana hawa
watapatiwa vyeti,
wataunganishwa na kuunda
kikundi ama taasisi itakayo
husika na kutoa
mafunzo ya ujasiriamali
kwa wajasiriamali wadogo
wadogo waliopo katika
kata wanazo
ishi.
Kikundi hicho
kitaingizwa katika MTANDAO
WA WAALIMU WA
UJASIRIAMALI TANZANIA na
kunufaika na fursa
mbalimbali zitakazo tolewa
chini mtandao.
Hii ni
fursa ya kipekee
kwa vijana wa kitanzania
waishio jijini Dar
Es salaam wenye
elimu ya kuanzia
kidato cha nne
na kuendelea.
Fikeni katika
Chuo Chetu kwa
ajili ya kujiandikisha
katika mafunzo ya
bure kabisa ya
UALIMU WA UJASIRIAMALI
yatakayo wajengea uwezo wa
kuwasaidia kujiajiri kama
waalimu wa ujasiriamali.
Comments
Post a Comment