Skip to main content

NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI




NAFASI   ZA  MAFUNZO   NA  KAZI.
RafikiElimu  Foundation  ni  Taasisi  Isiyokuwa  ya  kiserikali  ( NGO )  inayo  jihusisha  na  Maendeleo  Ya  Sekta  ya  Elimu  Tanzania. Taasisi   inatangaza  nafasi  za  MAFUNZO   YA   UTENGENEZAJI   WA  VYAKULA  MAALUMU  KWA  WAGONJWA  WA  PRESHA  NA  KISUKARI,WAZEE, WAJAWAZITO, WATOTO  WACHANGA  NA  WATU   WENYE  MATATIZO  YA  UNENE & UZITO.  Lengo  la  mafunzo  haya  ni  kuwaandaa   wahitimu  kufanya  kazi  ya   kutoa  mafunzo  watakayo  yapata  kwa  vijana  Elfu  Tano  waliopo  katika  kata  mbalimbali  za  jijini  Dar  Es  salaam.
SIFA  ZA  KUJIUNGA  NA  MAFUNZO:
1.            Awe  na  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne, sita  na  kuendelea.
2.            Awe  mkaazi  wa  Dar  Es salaam.
3.            Awe  na  uwezo  wa  kuwasiliana  kwa  lugha  za  Kiswahili  na  kiingereza.

MUDA  WA  MAFUNZO :   Mafunzo  haya  yatafanyika  kwa  muda  wa  siku   tatu  kuanzia  tarehe  07 OKTOBA  2013  hadi  tarehe  09 Oktoba 2013  katika  ukumbi  wa  mikutano  wa  Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation  uliopo  katika  eneo la  CHANGANYIKENI  karibu   na  CHUO  CHA  TAKWIMU.

KUANZA  KAZI : Wahitimu   wote  wa  mafunzo  haya  wataanza  majukumu  yao  kuanzia  tarehe   14  OKTOBA  2013.
ADA  YA  MAFUNZO: Ada  ya   kushiriki  katika   mafunzo  haya  ni  SHILINGI  ELFU  ISHIRINI  NA  TANO  TU (  Tshs.25,000/-) 
FOMU  ZA  KUJIUNGA  NA  MAFUNZO: Fomu  za  kujiunga  na  mafunzo   haya  zinapatikana  kwa  SHILINGI  ELFU  KUMI  NA  MBILI  TU ( Tshs.12,000/-) katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.
Mwisho  wa  kuchukua  fomu  ni  tarehe  05 oktoba  2013.

Kufika   katika  ofisi  zetu  panda  daladala  za  UBUNGO-CHANGANYIKENI  kisha  shuka  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele  kisha  tazama  upande  wako  wa  kulia  utaona  ofisi  imeandikwa  RAFIKIELIMU  FOUNDATION.

           

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...