Taasisi ya RafikiElimu Foundation inapenda kuwatangazia vijana wa kitanzania nafasi za mafunzo na kazi kama ifuatavyo :
KOZI ITAKAYO FUNDISHWA : NGO MANAGEMENT & OPERATION.
SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI :
1. Kijana wa kitanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 45.
2. Elimu ya kuanzia kidato cha sita na kuendelea.
3. Aliye na malengo ya kufanya kazi katika taasisi zisizokuwa za kiserikali zilizopo nchini Tanzania.
4. Anayeweza kusoma na kuelewa kwa njia ya masafa marefu.
LENGO LA KOZI HII :
i.
kumuandaa mhitimu kufanya
kazi katika taasisi
zisizo kuwa za kiserikali
katika maeneo ya
ubunifu, uandishi na usimamizi
wa miradi yenye
kuvutia na kushawishi
wafadhili
(
Designing, Developing & Managing
Donor Funded Projects
)
ii.
Kumuandaa mwanafunzi kufanya
kazi kwa ufanisi mkubwa katika
taasisi zisizokuwa za kiserikali
katika maeneo ya
utafutaji na utengenezaji
wa fedha za
kukuza mfuko wa
taasisi husika.
( Designing,
Managing & Developing Fund Raising
Programmes )
iii.
Kumuandaa mwanafunzi
kufanya kazi kwa
ufasaha mkubwa katika
taasisi zisizokuwa za
kiserikali kama mtafiti
wa tafiti za
aina mbalimbali kama
vile tafiti za
kijamii, tafiti za mazingira, tafiti za
kisheria nakadhalika.
iv.
Kumuandaa mwanafunzi
kufanya kazi katika
taasisi zisizokuwa za kiserikali
kama msimamizi na
mratibu wa miradi
na shughuli mbalimbali
za taasisi husika.
v.
Kumuandaa mwanafunzi
kufanya kazi katika
taasisi zisizo kuwa
za kiserikali kama
mwalimu wa somo
la ujasirimali, uongozi wa
biashara pamoja na utengenezaji wa
bidhaa za aina
mbalimbali kwa njia
ya nadharia kama
vile sabuni, chaki, mishumaa,
batiki nakadhalika.
vi.
Kumuandaa mwanafunzi
kufanya kazi kama
msimamizi wa shughuli za katika
taasisi zisizokuwa za
kiserikali zinazojihusisha na
masuala ya uwekaji na
ukopaji wa pesa
( VICOBA & SACCOSS ) pamoja
na usimamizi wa
uundwaji wa taasisi
za aina hiyo.
vii.
Kumuandaa mwanafunzi
kufanya kazi katika
taasisi mbalimbali kama
mtoa elimu ya ukimwi, mazingira na uraia. n.k.
MUDA WA MAFUNZO : Mafunzo haya yatafanyika kwa muda wa miezi mitatu. Mwezi mmoja utakuwa ni mafunzo kwa njia ya nadharia na miezi miwili itakuwa ni mafunzo kwa njia ya vitendo ambayo yatafanyika katika taasisi zisizo kuwa za kiserikali.
BAADA YA KUHITIMU : Wahitimu wa mafunzo haya, watapata nafasi ya kufanya " internship " kwa muda wa miezi sita, katika miradi mbalimbali inayo ratibiwa na taasisi mbali mbali zisizokuwa za kiserikali nchini Tanzania kwa kutumia ujuzi walioupata katika mafunzo haya.
ADA YA MAFUNZO : Ada ya mafunzo haya ni nafuu sana.
Tuma maombi ya fomu ya kujiunga na mafunzo-kazi haya kupitia barua pepe yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.comm.
Maombi yaelekezwe kwenda kwa :
Mkurugenzi Mtendaji,
RafikiElimu Foundation,
Centre For Distance Learning Programme.
S.L.P 35967,
Dar Es salaam.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 08 JANUARY 2013.
Mafunzo yataanza, tarehe 14 JANUARY 2013.
Tunapokea maombi kutoka waombaji waliopo katika wilaya zote za Tanzania Bara.
Tunapokea maombi kutoka waombaji waliopo katika wilaya zote za Tanzania Bara.
Comments
Post a Comment