Skip to main content

Mradi Wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini Kuzinduliwa tarehe 01 NOVEMBA 2012.

Mradi  Wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini " EUMIVI -Project  " , unao  ratibiwa  na  Taasisi  Isiyokuwa  ya  kiserikali  ya  RafikiElimu  Foundation(  RAEFO  TANZANIA )   unatarajia  kuzinduliwa  rasmi  tarehe  01  NOVEMBA  2012,  kwenye  Ukumbi  wa  HEKO  HALL, uliopo  katika  eneo  la  SINZA - AFRIKA  SANA  jijini  Dar  Es  salaam.

Akiteta  na  RAFIKIELIMU  BLOG ,  Msemaji  wa  Taasisi  ya  RAEFO  TANZANIA , Ndugu  Consolatha  THADEUS  amesema  ya  kuwa  ingawa  mradi  utazinduliwa, siku  ya  tarehe  01  NOVEMBA  2012, saa  tisa  kamili  Alasiri  lakini  mafunzo  yatakuwa   yakifanyika  asubuhi  na  mchana na  yatakuwa  yakifanyika  kila  siku  kwa  muda  wa  miezi  miwili  ambapo  kwa  kuanza,  wanafunzi  watapatiwa  mafunzo  kwa  njia  ya  nadharia   katika  awamu  ya  kwanza  kisha  kumalizia  na  mafunzo  kwa  njia  ya  vitendo  katika  awamu  ya  pili ya  mafunzo.

"  Tumeamua kuyafanya  mafunzo  asubuhi  na  jioni  ili  kuwapa  nafasi  watokao  makazini  ambao  mara nyingi  wanakuwa  hawana  nafasi  wakati  wa  asubuhi  na  mchana  kutokana  na  kubanwa  na  majukumu  kazini"  Alisema   Dada  CONSOLATHA  THADEUS.

" Mafunzo  yatakuwa  yakifanyika  katika  utaratibu  na  ratiba  ifuatayo  :  Wanafunzi  watagawanywa  katika  makundi  makuu  mawili, kundi la  kwanza  litasoma  kati  ya  Saa  3 kamili  asubuhi  hadi  saa  sita  kamili  mchana  na  kundi  la  pili  litakuwa  likisoma  kati  ya  saa  9  kamili  alasiri  hadi  saa  12  kamili  jioni "  aliongeza. Ms  THADEUS.

Mradi  wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini,  ni  Mradi  ambao  umelenga    kupambana  na  tatizo  la  ukosefu  wa  ajira  nchini  kwa  kutoa  elimu  ya  ujasiriamali  kwa  watu  wa  kada  mbalimbali  katika  jamii  kama  vile, vijana, wakina  mama  wajane, wakina  mama  na  vijana  walio  katika  vikundi  vya  uzalishaji,  wastaadu na  wanaop  jiandaa  kustaafu, wanafunzi  wa  mashuleni  na  vyuoni,   wanachama wa  VICOBA  na  SACCOSS  mbalimbali  nakadhalika.

Mafunzo  katika  mradi  huu  yatatolewa  bure  na  yataanza  rasmi  tarehe  01  NOVEMBA  2012.

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...