Skip to main content

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOLEWA BURE

Taasisi  Isiyokuwa  ya  Kiserikali  ya  RafikiElimu  FOUNDATION  kupitia  Mradi  wake   ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI &  VIJIJINI  “ EUMIVI-Project “  inapenda  kuwatangazia  vijana  wote  wa  kitanzania  wenye  umri  wa  kati  ya  miaka  kumi  na  tano ( 15 )  hadi     Arobaini  na  Tano  (   45  )   nafasi  za  kushiriki  katika  mafunzo  ya  ujasiriamali.
Mafunzo  yatakayo  tolewa  ni  pamoja  na :
i.                    Utengenezaji  na  Uzalishaji  wa  Bidhaa  za  aina  mbalimbali  kama  vile  :
a.    sabuni  za  aina  zote
b.     batiki
c.      chaki  za  aina  zote.
d.    Mishumaa.
e.    usindikaji   wa  vyakula, vinywaji& matunda
f.       Uokaji  wa  mikate,
g.    utengenezaji  wa  bidhaa  za  ngozi  kama  vile  mikanda  na  viatu  kwa  kutumia  ngozi  za  wanyama  zilizo  sindikwa.
h.    Utengenezaji  wa  viungo  vya  vyakula  vya  binadamu  kama  vile  Chilli  Sauce, Tomato Sauce, Mango Picco , Peanut Butter nakadhalika.
i.       Utengenezaji  wa   mkaa  kwa  kutumia  makaratasi.
j.       Utengenezaji  wa  kiwi.
k.    Utengenezaji  Wa  Vyakula   Vya  Mifugo  kama  vile  kuku na  n’gombe.
l.       Mbinu  Za  Ufuaji  Bora.
m. Mbinu  za  kilimo  Bora.
ii.                Elimu  Ya  Ujasiriamali.
iii.              Elimu  Ya   Sheria  Za  Biashara.
iv.              Elimu  Ya  Usimamizi  na  Uongozi  Wa  Biashara.
v.                Ubunifu, Uendeshaji  na  Usimamizi  Wa  Miradi
vi.              Uandishi  Wa  Miradi Mbalimbali.
vii.           Elimu  Ya  Uwekaji  na Ukopaji  Fedha  .
viii.         Elimu  Ya  Uendeshaji  wa  Vikundi  Vidogo  Vidogo  Vya  Kuweka  na  kukopa   Fedha.
ix.              Elimu  Ya  Utengenezaji  na  Utafuta  wa  Masoko.

ADA  YA  USAJILI :  Ada  ya  kujisajili  katika  mradi  huu  ni  BURE.
ADA  YA  MAFUNZO :  Ada  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  ni  BURE.
MWISHO   WA  KUJIANDIKISHA  : Tarehe  25  OKTOBA  2012.
KUANZA   KWA  MAFUNZO    :   Tarehe    01  NOVEMBA  2012.
KUZINDULIWA  KWA  MRADI  :  Tarehe  23  OKTOBA  2012.

NAMNA  YA  KUJIANDIKISHA :  Fika  katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.
Panda  gari  za  UBUNGO  -  CHANGANYIKENI,  kisha   shuka  kituo  kinaitwa  TAKWIMU. Ukifika  TAKWIMU    fuata  barabara  ya  lami  hatua  ishirini ( 20 )  kisha  tazama  upande  wako  wa  kulia  utaona  bango  la  ofisi  yetu  limeandikwa  RAFIKIELIMU  FOUNDATION.

Kwa    maelezo  zaidi  wasiliana  nasi  kwa  simu
               0763976548    AU    0782405936.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  Mradi  Huu, tembelea  blogu  yetu :  www.rafikielimu.blogspot.com

WAHI  NAFASI  YAKO  MAPEMA  KWANI  NAFASI  ZILIZOPO  NI  CHACHE.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...