NAFASI ZA KAZI ( FOOD PRODUCTION )
RafikiElimu Education Consultancy ni Taasisi
inayo jihusisha na usimamizi wa maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wanao soma
katika shule za msingi na sekondari nchini Tanzania, pamoja na mafunzo ya ujasiriamali. Taasisi Kwa kushirikiana na shule mbalimbali za msingi na sekondari katika
mikoa ya Dar Es Salaam na Mtwara inaratibu
mradi wa “ MAFUNZO YA UTENGENEZAJI
WA PIPI ZA VIJITI” almaarufu kama “ PIPI ZA KIHINDI”, kwa vijana
waliomaliza kidato cha nne. Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea vijana hao , uwezo wa kujiajiri wenyewe kwa kutengeneza na kuuza pipi hizo kwenye shule za msingi na
sekondari ambazo zinashirikiana na taasisi
katika mradi huu. Kupitia mradi
huu, taasisi inatangaza nafasi za kazi ya
kufundisha namna ya kuandaa na kutayarisha pipi za vijiti ( Pipi za
kihindi ). Mafunzo haya yatatolewa kwa
vijana wanao simamiwa na taasisi yetu
katika mradi huu.
SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI :
1.
Awe na elimu ya kuanzia ngazi ya cheti katika
fani ya FOOD PRODUCTION kutoka katika chuo kinacho tambuliwa na serikali au AWE
Mwanafunzi anae chukua kozi ya FOOD PRODUCTION kuanzia ngazi ya cheti na
kuendelea.
2.
Awe wa jinsia yoyote mwenye uwezo mkubwa wa kujielezea na kuelekeza.
3.
Awe maridadi,mwaminifu, mwenye bidii na nidhamu.
IDADI YA NAFASI
: idadi ya nafasi za kazi zilizopo
kwenye mradi huu ni nafasi kumi na saba ( 17)
MUDA WA MRADI : Mradi huu utafanyika kwa muda wa miezi sita kuanzia tarehe 02 DESEMBA 2024.
MAJUKUMU YA KAZI : Majukumu ya kazi kwa watakao fanikiwa
kupata nafasi hii yatakuwa ni kutoa mafunzo ya jinsi ya kutengeneza pipi za
vijiti, pamoja na kuwasimamia wahitimu wa mafunzo hayo kwenye vituo vyao vya
kazi.( Mashuleni )
Waombaji watakao pata nafasi hii ya kazi watapewa semina
maalumu itakayo wajengea uwezo wa kufanya kazi katika mradi huu kama wakufunzi
wa mafunzo ya kutengeneza pipi za vijiti.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Maombi yote yatumwe kupitia barua pepe yetu ambayo ni: rafikielimutanzania@gmail.com. Maombi yote yaambatanishwe na CV pamoja na
passport size ya rangi.
MWISHO WA KUTUMA
MAOMBI : Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 31 OCTOBER 2024.
Kwa maelezo zaidi:
Tutembelee kupitia tovuti yetu : www.rafikielimu.blogspot.com
Comments
Post a Comment