Skip to main content

RC Chalamila: Dar es Salaam kufuta shule zote za sekondari za kutwa ili kudhibiti nidhamu ya wanafunzi





Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wapo kwenye mchakato wa kufuta shule zote za sekondari za kutwa kwa ajili ya kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi wote wa sekondari. Chalamila ameyasema hayo katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Azania kwenye hafla ya kukabidhi magari kwa maafisa elimu wa sekondari kutoka wilaya nane, ambapo amesema, Mkoa wa Dar es Saalam una shule za sekondari 182 na za binafsi zipo nyingi zaidi ya 200. --- ILI kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wapo kwenye mchakato wa kufuta shule zote za Sekondari za kutwa. Chalamila ameyasema hayo leo Agosti 14, 2023 katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Azania kwenye hafla ya kukabidhi magari kwa maafisa elimu wa sekondari kutoka wilaya nane. Amesema, Mkoa wa Dar es Saalam una shule za sekondari 182 na za binafsi zipo nyingi zaidi ya 200. “Katika Mkoa tunapokea sh billion 1.3 fedha zinazohudumia wanafunzi kama ada na posho ya madaraka kwa walimu. Amesema, pamoja na kwamba Dar es Salaam ina shule nyingi, kidato cha sita ndio inafanya vizuri katika matokeo lakini kidato cha nne bado ni changamoto kwa sababu kuna shule nyingi sio za bweni. ” Na kwa sababu ya vitendo vingi vinavyoendelea mitaani ikiwemo ukosefu wa maadili, foleni sisi tumeshakaa kikao chetu na shule zetu, tumepanga mipango kwamba sasa tujipe muda tuanze kufuta shule za kutwa ili hapa katikati kote tuwe na shule za bweni tu..”, mesema Chalamila na kuongeza “Tutafuta shule za kutwa tubaki na Bweni hii itasaidia kumanage nidhamu ya wanafunzi katika makuzi yao lakini pia muda wanaofika shule na hata walimu wa ziada ni rahisi kuweza kuwamanage wanapokuwa pamoja. “Tutakuletea concept mezani mh Waziri ( Angela Kairuki – Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi) kwako ili kama kuna wafadhili basi wafikirie pia Mkoa wetu, si tu kuwa na shule nyingi ni kwamba una wanafunzi pia wengi.” Amesema Aidha, Chalamila ameomba shule zote za Dar es Salaam kufungiwa umeme wa Sola kupitia miradi mbali mbali ya Tarura. ” Mh Waziri kwenye haya mashule badala ya kutumia umeme wa gridi ya taifa, program ya barabara za Tarura kuna ‘package’ ya taa, naomba angalau kupata taa 10 kwa kila shule zikafungwa ili kupunguza adha ya kulipa bili ya umeme kwa hizi shule na kuwapunguzia gharama Chanzo: Habari Leo

Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...