Skip to main content

NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI


Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation   inapenda  kuwatangazia  vijana  wa  kitanzania  nafasi  za  mafunzo  na  kazi  kama  ifuatavyo :

KOZI  ITAKAYO  FUNDISHWA : USIMAMIZI  & UENDESHAJI  WA  TAASISI  ZISIZOKUWA  ZA  KISERIKALI   
(  NGO  MANAGEMENT & OPERATION )

SIFA  ZA  MWOMBAJI  NAFASI :

      1. Kijana  wa  kitanzania  mwenye  umri  wa  kati  ya  miaka  18 hadi 45.
2. Elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne, sita  na  kuendelea.
3. Aliye   na  malengo  ya  kufanya  kazi  katika  taasisi  zisizokuwa  za  kiserikali  zilizopo  nchini  Tanzania.
4 . Awe  anaishi  katika  wilaya  yoyote  iliyopo  Tanzania  bara
4. Anayeweza  kusoma  na  kuelewa  kwa  njia  ya  masafa  marefu. 


LENGO  LA  KOZI  HII :


i.                   kumuandaa  mhitimu   kufanya  kazi  katika  taasisi  zisizo  kuwa za  kiserikali   katika  maeneo  ya    ubunifu, uandishi  na  usimamizi  wa  miradi  yenye  kuvutia  na  kushawishi  wafadhili
( Designing, Developing & Managing Donor  Funded  Projects  )

ii.                 Kumuandaa  mwanafunzi  kufanya  kazi  kwa  ufanisi mkubwa   katika  taasisi zisizokuwa  za  kiserikali  katika  maeneo  ya  utafutaji  na  utengenezaji  wa  fedha   za  kukuza  mfuko  wa  taasisi  husika.

(  Designing, Managing & Developing  Fund  Raising  Programmes  )


iii.              Kumuandaa  mwanafunzi  kufanya  kazi  kwa  ufasaha  mkubwa  katika  taasisi  zisizokuwa   za  kiserikali   kama   mtafiti  wa  tafiti  za  aina  mbalimbali  kama  vile  tafiti  za  kijamii, tafiti  za  mazingira, tafiti  za  kisheria  nakadhalika.
iv.              Kumuandaa   mwanafunzi  kufanya  kazi  katika  taasisi  zisizokuwa  za kiserikali  kama  msimamizi  na  mratibu  wa   miradi  na  shughuli  mbalimbali  za  taasisi  husika.

v.                 Kumuandaa  mwanafunzi  kufanya  kazi  katika  taasisi  zisizo  kuwa  za  kiserikali  kama  mwalimu  wa  somo  la  ujasirimali, uongozi  wa  biashara  pamoja  na  utengenezaji  wa  bidhaa  za  aina  mbalimbali  kwa  njia  ya  nadharia  kama  vile  sabuni, chaki, mishumaa, batiki  nakadhalika.

vi.              Kumuandaa  mwanafunzi   kufanya  kazi  kama  msimamizi  wa shughuli  za   katika  taasisi  zisizokuwa  za  kiserikali  zinazojihusisha  na  masuala  ya  uwekaji  na  ukopaji  wa  pesa   ( VICOBA  & SACCOSS )  pamoja  na  usimamizi  wa  uundwaji  wa  taasisi  za  aina  hiyo.

vii.            Kumuandaa  mwanafunzi  kufanya  kazi  katika  taasisi  mbalimbali  kama  mtoa  elimu  ya  ukimwi, mazingira  na  uraia. n.k.


MUDA  WA  MAFUNZO : Mafunzo  haya  yatafanyika  kwa  muda  wa  miezi  mitatu.  Mwezi  mmoja  utakuwa  ni  mafunzo  kwa  njia  ya  nadharia  na  miezi  miwili  itakuwa  ni  mafunzo  kwa  njia  ya  vitendo  ambayo  yatafanyika  katika  taasisi  zisizo  kuwa  za  kiserikali.

BAADA  YA  KUHITIMU : Wahitimu  wa  mafunzo  haya, watapata  nafasi  ya  kufanya  " internship "  kwa muda  wa  miezi  sita, katika  miradi  mbalimbali inayo  ratibiwa na  taasisi mbali mbali  zisizokuwa  za  kiserikali  nchini  Tanzania  kwa  kutumia  ujuzi  walioupata  katika  mafunzo  haya.

ADA  YA  FOMU  YA  MAOMBI : Ada  ya  fomu  ya  maombi  ni  SHILINGI  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU. ( Tshs.15,000/)
ADA  YA  MAFUNZO  : Ada  ya  mafunzo  haya  ni  nafuu  sana.




Tuma  maombi   ya  fomu  ya  kujiunga  na  mafunzo-kazi  haya   kupitia  barua  pepe yetu  ambayo  ni :  rafikielimutanzania@gmail.com.
  
AU   
Fika  moja  kwa  moja  katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.

Maombi  yaelekezwe  kwenda  kwa  :
Mkurugenzi  Mtendaji,
RafikiElimu  Foundation,
Centre  For  Distance  Learning  Programme.
S.L.P  35967,
Dar  Es  salaam.

Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe  31 JANUARY 2014.

Mafunzo  yataanza, tarehe  03  FEBRUARI  2014.

Tunapokea  maombi  kutoka  waombaji  waliopo  katika  wilaya  zote  za  Tanzania  Bara.



Comments

Popular posts from this blog

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe. UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa...

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.  Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka. MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI. * Nanasi. *  Maji. * Sukari. * Amira. HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA *  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  ) *  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  n...

SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE.

 MASOMO  YATAKAYO  FUNDISHWA  HAPA  NI : 1 1. Utengenezaji  Wa Sabuni  isiyo na garama. 22. Utengenezaji  Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji  Wa  Sabuni ya asali na cream. 4 4.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya manukato. 5 5.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ngumu. 66.  Utengenezaji   Wa  Sabuni ya unga 77. Utengenezaji   Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji    Wa  Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji  Wa  Sabuni za rangi. 110.  Utengenezaji  Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji  Wa  Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine.  VIFAA     VYA     UTENGENEZAJI   SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mwiko.  *Chombo chenye ukubwa cha plastiki. *Kifyatulio. *Ki...