Wanafunzi wa shule ya sekondari. Jumla ya wanafunzi 438,960 kati ya wanafunzi 451,392 waliofaulu mtihani wa darasa la saba nchini Tanzania wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali za sekondari kwa awamu ya kwanza. 0 Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa Akitangaza matokeo ya ufaulu huo kwa vyombo vya habari na wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.23 ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo. Naibu waziri, Majaliwa amesema kati ya wanafunzi waliochaguliwa wasichana ni 219,996 sawa na asilimia 97.1 na wavulana 218964 sawa na asilimia 97.28 na kuon...