Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2013

AWEP TANZANIA YAZINDULIWA RASMI

 African Women Entreprenuership Programme (AWEP) Tanzania Chapter imezinduliwa rasmi jioni hii katika hoteli ya Double Tree,mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda ,pamoja na Balozi wa Marekani nchini  Alfonso Lenhardt  Hii ni Ngao iliyobidhiwa rasmi na Sylvia Banda  ambaye ni balozi na mwenyekiti wa AWEP Zambia ,kudhihirisha kuwa AWEP Tanzania imezinduliwa rasmi kwa kuikabidhi kwa Mgeni rasmi wa Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda na Balozi wa Marekani nchini ,Alfonso Lenhardt  Madam Sylvia Banza, Balozi wa AWEP Zambia akiikabidhi ngao hii , ambayo nae alikabidhiwa na Mama Bill Clinton alipoizindua AWEP Zambia mwaka juzi                                          Mwenyekiti wa AWEP Tanzania, Bi Flotea Masawe.               Bal...

DARASA LA SABA KUDAHILIWA VYUO VIKUU.

Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao. Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu. Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B. Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu. Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine. Sifa zinazo...

KUHUSU VITUO VYA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WA INTAKE YA MWEZI MACHI.

Uongozi  wa  RafikiElimu  Foundation  unapenda  kuwajulisha  wanafunzi  wetu wote  wanao  chukua  mafunzo  ya  NGO-MANAGEMENT & OPERATION   ( MARCH  INTAKE )  na  wale  wanao  soma  mafunzo  ya  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI   kuwa  wameisha  tumiwa  kwa  njia  ya  barua  pepe, barua  za  kuripoti  katika  vituo  vyao  vya  mafunzo  kwa  vitendo.  Kwa wanafunzi  ambao  mpaka  sasa  bado  hawajapokea  barua  za  kuripoti  katika  vituo  vya  mafunzo  kwa  vitendo  mnaombwa  kutujulisha  kwa  barua  pepe  ama  kupiga  simu  namba 0782405936. Atakaye  pokea  ujumbe  huu, anaombwa  kumfahamisha  na  mwenzake. Imetolewa  na  Uo...

MAMBO 10 MUHIMU YA KUFAHAMU KUHUSU shuledirect.co.tz YA FARAJA NYALANDU

            Naibu Waziri wa Elimu Philipho Mulugo ndio alikua mgeni rasmi.      1. Faraja Nyalandu ambae alikua Miss Tanzania 2004 maarufu kama Faraja Kota ndio mwanzilishi wa mfumo wa Wanafunzi Tanzania  kujisomea masomo mbalimbali kupitia Internet kupitia shuledirect.o.tz . 2. Ni mfumo wa kitaaluma wa Wanafunzi, ni zaidi ya mtandao wa kawaida kwa sababu pamoja na kwamba ukiingia unaweza kusoma masomo mbalimbali, pia unaweza kuchat na watu mbalimbali, 3. Masomo yanayopatikana ni ya Sekondari kuanzia form I mpaka IV. 4. Mwanafunzi anayo nafasi ya kuchat na walimu, kuuliza maswali na kujibiwa, 5. Mpango wa kuongeza walimu upo, kwa sasa wako tisa ambapo kila mmoja anayo degree na uzoefu usio wa chini ya miaka mitano, 6. Kutakua na Quiz ambayo Mwanafunzi anaweza kujibu na ikasahihishwa na Walimu na kurudishiwa majibu. 7. Wizara ya Elimu imeridhia na kuipa baraka zote shuledirect.co.tz...

Laws of Tanzania (CD-ROM) (Principal and subsidiary legislation revised edition 2002

      This is the first complete revision of the laws of Tanzania since 1966 and comprises principal legislation and subsidiary legislation in force on 31 July 2002. The principal legislation consists of 415 chapters arranged numerically. There are ten main volumes and a supplementary volume, which contains the index, alphabetical and chronological tables and certain omitted Acts which were not in force at the completion of the Law Revision of 2002. The revised edition of the subsidiary legislation has been arranged in a similar fashion and consists of ten volumes. The edition consists of various tables of content; the Constitution (in Kiswahili); and the ordinary laws of the country (Acts and subsidiary legislation), set out in numbered chapters. *Contents Include:*    - Statutes of Tanzania, revised edition 2002    - Principal legislation consisting of 415 Chapters in 10 volumes    - Supplementary Volume with alp...

MASAA 24 YA MLEMAVU WA MACHO UDSM!

Pichani ni Vicent Mzena(Mwenye fimbo nyeupe)  MASAA 24 YA MLEMAVU WA MACHO UDSM! Hi sehemu ya makala yangu kwenye gazeti la RAI no 978 ...... Binafsi sipingi kuanzishwa kwa mfumo shirikishi. Kwa mtazamo wangu, mfumo shirikishi una faida anuai. Mosi, unawaandaa wanafunzi walemavu kuchanganyika na jamii ambayo kimsingi ndiyo wataishi nayo uraiani. Pili, unawapa fursa wanafunzi wasio walemavu kufahamu changamoto, fursa na mahitaji ya walemavu. Pia mfumo shirikishi unasemwa kuongeza fursa kwa walemavu wengi zaidi kupata elimu kwa sababu una gharama nafuu. Hili la mwisho linahitaji utafiti zaidi. Jambo la msingi ambalo tunapaswa kujiuliza ni kama wanafunzi wasio na ulemavu na jamuiya za taasisi za elimu kama vile shule na vyuo zimejiandaa kikamilifu kuishi kwa upendo na walemavu na kufahamu vyema mahitaji yao. Nasema hivyo kwa sababu elimu shirikishi haiwezi kufanikiwa kwa kiwango kinachotarajiwa kama jamii itakuwa haijaandaliwa vizuri kisaikolojia...

TANGAZO KWA WANAFUNZI WETU WA UALIMU WA UJASIRIAMALI

Tunapenda  kuwatangazia  wanafunzi  wetu  wote  wa  kozi  ya  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI  inayo  tolewa   chini  Mradi  Wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini  ( EUMIVI  -Project  )  kwamba  wanatakiwa  kuwa  wamekwisha  pokea  maswali  ya  mitihani  ya  nadharia  mpaka  sasa.  Kwa  wanafunzi  ambao  mpaka  sasa  bado  hawajapokea   maswali  ya  mtihani  wa   nadharia   tafadhali  tuandikieni  barua  pepe    ya  kutujulisha. Imetolewa  na  Uongozi, RafikiElimu   Foundation.