NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU WA UJASIRIAMALI.
( INTAKE HII
NI MAALUMU KWA
WAOMBAJI WANAOTAKA KUWA
WAALIMU WA UJASIRIAMALI
KATIKA MRADI WA
ELIMU YA UJASIRIAMALI
MIJINI & VIJIJINI KWENYE
WILAYA WANAZO ISHI )
Taasisi ya RafikiElimu
Foundation inapenda kuwatangazia vijana
wa kitanzania nafasi za mafunzo na
kazi kama ifuatavyo :
KOZI ITAKA YO FUNDISHWA :
UALIMU WA
UJASIRIAMALI.
SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI :
1. Awe mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45.
2.Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne,
sita na kuendelea.
3. Aliye na utashi na malengo ya kufanya
kazi kama MWALIMU
WA UJASIRIAMALI kwenye
Mradi Wa Elimu
Ya Ujasiriamali Mijini
& Vijijini.
4. Anayeweza kusoma na kuelewa kwa
njia ya masafa marefu.
5. Awe anaishi
katika wilaya yoyote iliyopo Tanzania bara.
DHUMUNI LA KOZI HII : Dhumuni kuu la mafunzo haya ni kuwaandaa wahitimu kufanya kazi kama WAALIMU WA UJASIRIAMALI katika Mradi Wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini unaoratibiwa na Taasisi.
MUDA WA MAFUNZO : Mafunzo haya
yatafanyika kwa muda wa miezi mitatu.
Mwezi mmoja utakuwa ni mafunzo kwa
njia ya nadharia na miezi miwili
itakuwa ni mafunzo kwa njia ya vitendo
ambayo yatafanyika mashuleni na
kwenye vituo vya
mafunzo ya ujasiriamali.
BAADA YA
KUHITIMU : Wahitimu wa mafunzo haya, watapata
nafasi ya kufundisha somo
la Ujasiriamali mashuleni na katika vituo vya
ujasiriamali vilivyopo katika
wilaya zao. .
ADA YA MAFUNZO: Ada ya mafunzo
haya maalumu ni shilingi elfu
35 tu kwa mwezi.
Tuma maombi ya fomu ya
kujiunga na mafunzo-kazi haya kupitia
barua pepe yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.com.
Maombi
yaelekezwe kwenda kwa :
Mkurugenzi Mtendaji,
RafikiElimu Foundation,
Centre For
Distance Learning Programme.
S.L.P 35967,
Dar Es salaam.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe
08 MACHI
2013.
Mafunzo yataanza, tarehe 14 MACHI 2013.
N.B: Tutachukua wanafunzi
wachache kutoka katika
wilaya hivyo idadi
ya wanao hitajika
ikikamilika mapema,
tutasitisha kupokea maombi
mapya.
Comments
Post a Comment