Total Pageviews

Monday, April 29, 2013

AWEP TANZANIA YAZINDULIWA RASMI

 African Women Entreprenuership Programme (AWEP) Tanzania Chapter imezinduliwa rasmi jioni hii katika hoteli ya Double Tree,mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda ,pamoja na Balozi wa Marekani nchini  Alfonso Lenhardt
 Hii ni Ngao iliyobidhiwa rasmi na Sylvia Banda  ambaye ni balozi na mwenyekiti wa AWEP Zambia ,kudhihirisha kuwa AWEP Tanzania imezinduliwa rasmi kwa kuikabidhi kwa Mgeni rasmi wa Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda na Balozi wa Marekani nchini ,Alfonso Lenhardt
 Madam Sylvia Banza, Balozi wa AWEP Zambia akiikabidhi ngao hii , ambayo nae alikabidhiwa na Mama Bill Clinton alipoizindua AWEP Zambia mwaka juzi
                                         Mwenyekiti wa AWEP Tanzania, Bi Flotea Masawe.


              Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt,  ambao ni wafadhili  wa AWEP  katika mkakati wake wa kuwakwamua wanawake  wajasiriamali wa Afrika
                    Waziri Abdallah Kigoda akiwasili katika hafla ilofanyika jioni hii, na kuhudhuriwa na wanachama kutoka sehemu mbalimbali nchini, ambao baadhi walikuwa katika mafunzo ya kujifunza ujasiri amali ambao unalengo la kuwafanya wawekezaji

Mama Lowasa pamoja na Balozi Maajar walihudhuria uzinduzi huu wa AWEP Tanzania
Baadhi ya wanachama wa AWEP Tanzania Chapter katika picha ya pamoja na mgeni rasmi sambamba na Balozi Alfonso

burudani ilikuwa toka kwa Makumbusho Traditional Dancers
 
                 CREDIT :  WWW.LADYJAYDEE.BLOGSPOT.COM

Sunday, April 21, 2013

DARASA LA SABA KUDAHILIWA VYUO VIKUU.

Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.

Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.

Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.

Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.

“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.

Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na kuongeza:

“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”

Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.

Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.

“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Wednesday, April 17, 2013

KUHUSU VITUO VYA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WA INTAKE YA MWEZI MACHI.

Uongozi  wa  RafikiElimu  Foundation  unapenda  kuwajulisha  wanafunzi  wetu wote  wanao  chukua  mafunzo  ya  NGO-MANAGEMENT & OPERATION   ( MARCH  INTAKE )  na  wale  wanao  soma  mafunzo  ya  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI   kuwa  wameisha  tumiwa  kwa  njia  ya  barua  pepe, barua  za  kuripoti  katika  vituo  vyao  vya  mafunzo  kwa  vitendo.  Kwa wanafunzi  ambao  mpaka  sasa  bado  hawajapokea  barua  za  kuripoti  katika  vituo  vya  mafunzo  kwa  vitendo  mnaombwa  kutujulisha  kwa  barua  pepe  ama  kupiga  simu  namba 0782405936. Atakaye  pokea  ujumbe  huu, anaombwa  kumfahamisha  na  mwenzake.

Imetolewa  na  Uongozi,
RafikiElimu  Foundation.

Thursday, April 11, 2013

MAMBO 10 MUHIMU YA KUFAHAMU KUHUSU shuledirect.co.tz YA FARAJA NYALANDU.
            Naibu Waziri wa Elimu Philipho Mulugo ndio alikua mgeni rasmi.
    
1. Faraja Nyalandu ambae alikua Miss Tanzania 2004 maarufu kama Faraja Kota ndio mwanzilishi wa mfumo wa Wanafunzi Tanzania  kujisomea masomo mbalimbali kupitia Internet kupitia shuledirect.o.tz .
2. Ni mfumo wa kitaaluma wa Wanafunzi, ni zaidi ya mtandao wa kawaida kwa sababu pamoja na kwamba ukiingia unaweza kusoma masomo mbalimbali, pia unaweza kuchat na watu mbalimbali, 3. Masomo yanayopatikana ni ya Sekondari kuanzia form I mpaka IV.
4. Mwanafunzi anayo nafasi ya kuchat na walimu, kuuliza maswali na kujibiwa, 5. Mpango wa kuongeza walimu upo, kwa sasa wako tisa ambapo kila mmoja anayo degree na uzoefu usio wa chini ya miaka mitano, 6. Kutakua na Quiz ambayo Mwanafunzi anaweza kujibu na ikasahihishwa na Walimu na kurudishiwa majibu.
7. Wizara ya Elimu imeridhia na kuipa baraka zote shuledirect.co.tz  8. shuledirect.co.tz ni huduma ya bure kwa kila mmoja, kinachotakiwa ni kujisajili tu, 9. Vinapatikana vitabu ambavyo wakati mwingine sio rahisi kupatikana mtaani, 10. kutakua kukifanyika mashindano kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo mijadala nia ikiwa pia ni kuitangaza zaidi shuledirect.co.tz
.
.
Kama na wewe umeguswa kumsupport Faraja, naomba nione like yako hapo chini pamoja na tweet yako ya hii post…. kwa info zaidi pia unaweza kumsikiliza Faraja Nyalandu akiongea hapa chini…

CREDIT:  WWW.MILLARDAYO.COM

Laws of Tanzania (CD-ROM) (Principal and subsidiary legislation revised edition 2002

 
 
 
This is the first complete revision of the laws of Tanzania since 1966 and
comprises principal legislation and subsidiary legislation in force on 31
July 2002. The principal legislation consists of 415 chapters arranged
numerically. There are ten main volumes and a supplementary volume, which
contains the index, alphabetical and chronological tables and certain
omitted Acts which were not in force at the completion of the Law Revision
of 2002. The revised edition of the subsidiary legislation has been
arranged in a similar fashion and consists of ten volumes. The edition
consists of various tables of content; the Constitution (in Kiswahili); and
the ordinary laws of the country (Acts and subsidiary legislation), set out
in numbered chapters.

*Contents Include:*

   - Statutes of Tanzania, revised edition 2002
   - Principal legislation consisting of 415 Chapters in 10 volumes
   - Supplementary Volume with alphabetical and chronological Table of Acts
   - Subsidiary Legislation consisting of 10 volumes

Pricing for single-user, main work archive only). Publication not updated.
Multiple-user pricing available on request.

*Of Interest and Benefit to:*

   - Judicial officers
   - Prosecutors
   - Legal practitioners
   - Libraries
   - Academics

*Key Benefits:*

   - Powerful electronic searching allows for easy and rapid access to
   information
   - Handy hyperlinks facilitate easy navigation within the product

ORDER TODAY!

contacts : WIGO
Mob: +255 655 308308,
        +255 767 102102,
email: cerengeti@gmail.com

MASAA 24 YA MLEMAVU WA MACHO UDSM!Pichani ni Vicent Mzena(Mwenye fimbo nyeupe)
 MASAA 24 YA MLEMAVU WA MACHO UDSM!
Hi sehemu ya makala yangu kwenye gazeti la RAI no 978

...... Binafsi sipingi kuanzishwa kwa mfumo shirikishi. Kwa mtazamo wangu, mfumo shirikishi una faida anuai. Mosi, unawaandaa wanafunzi walemavu kuchanganyika na jamii ambayo kimsingi ndiyo wataishi nayo uraiani. Pili, unawapa fursa wanafunzi wasio walemavu kufahamu changamoto, fursa na mahitaji ya walemavu. Pia mfumo shirikishi unasemwa kuongeza fursa kwa walemavu wengi zaidi kupata elimu kwa sababu una gharama nafuu. Hili la mwisho linahitaji utafiti zaidi.
Jambo la msingi ambalo tunapaswa kujiuliza ni kama wanafunzi wasio na ulemavu na jamuiya za taasisi za elimu kama vile shule na vyuo zimejiandaa kikamilifu kuishi kwa upendo na walemavu na kufahamu vyema mahitaji yao. Nasema hivyo kwa sababu elimu shirikishi haiwezi kufanikiwa kwa kiwango kinachotarajiwa kama jamii itakuwa haijaandaliwa vizuri kisaikolojia kuwapokea, kuwajali na kuwapenda walemavu.
Leo tutazame jinsi mfumo shirikishi unavyofanya kazi kwa mfano halisi; mfano wa maisha yangu. Mwaka 2011 ulikuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwangu kwenye siasa za chuo kikuu. Kwanza nilichaguliwa kuwa Katibu wa kitivo cha sheria na baadaye katibu wa bodi ya serikali ya wanafunzi(DARUSO). Kiongozi wa nafasi hiyo, ana fursa kubwa ya kupata sehemu nzuri ya malazi kwenye hosteli za chuo.
Mimi niliamua kuishi chumba kimoja na mlemavu wa macho Vicent Mzena ambaye naye alikuwa waziri wa Jinsia na makundi maalum katika serikali ya wanafunzi(DARUSO). Kuipokea changamoto ya kuishi chumba kimoja na mlemavu wa macho kumenipa ‘’uamsho’’ mkubwa. Mzena amekuwa mwalimu wangu mkubwa kuhusu mambo ya walemavu.
Somo la kwanza: Hapa tunajifunza kwamba jamii inapaswa kuchukulia kwamba kuishi na walemavu sio tatizo bali ni changamoto inayozalisha fursa ya kujifunza zaidi kutoka kwa walemavu na kuonyesha upendo kwao.
Ni asububuhi kumeshapambazuka. Mzena anaamka mapema. Chumba kimepangiliwa vyema na anafahamu ulipo mswaki, dawa ya meno na maji. Anakwenda mwenyewe bafuni kusafisha mwili. Mimi naamka na kumsaidia kunyoosha nguo zake alizozifua jana. Mzena ana desturi ya kufua nguo mwenyewe na kufuliwa mara chache hasa anapotingwa na majukumu.
Somo la pili: Hapa tunajifunza kwamba katika mfumo shirikishi, kila mmoja ana jukumu la kutekeleza. Walemavu wanapaswa kujizoesha kufanya wenyewe kazi ndogondogo wanazozimudu. Pia wanajamii wanaowazunguka walemavu wanajukumu la kuwasaidia kufanya kazi wasizoweza kuzitekeleza wenyewe.
Namshika mkono Mzena kumpeleka darasani ambaye mkononi ana fimbo nyeupe na begi la vifaa vya shule. Madarasa yako mbali kiasi. Mzena ni mcheshi sana. Tunacheka njia nzima huku akinitania kuwa mimi ni ‘’dereva mahiri’’. UDSM kuna jiografia ya milima lakini Mzena anajitahidi kuyazoea mazingira japo hapa na pale anatatizwa na ngazi.
Somo la nne: Hapa tunajifunza kwamba shule za mchanganyiko wa walemavu na watu wengine ziwe na miundombinu na mazingira rafiki kwa walemavu. Lakini pia walemavu wana jukumu la kuikabili changamoto ya mazingira yao kadiri inavyowezekana.

Kwenye varanda za hosteli na njiani kuelekea darasani tunakutana na wanafunzi wenzetu. Wanaonyesha kutujali na kutupisha njiani upesi. Lakini hapa kuna jambo la kuongeza. Wengi wanaonyesha kutunduwaa kwa mshangao. Baadhi yao wanasimamisha mazungumzo yao. Kwa ufupi,licha ya kuonyesha upendo na kujali, kuna kila dalili kwamba bado hawajaizoea kiukamilifu hali ya kujichanganya na walemavu.
Somo la tano: Hapa tunajifunza umuhimu wa kuijenga jamii kisaikolojia ili iweze kuwapokea walemavu kama sehemu ya jamii.
Sasa ni wakati wa kula. Mimi na mzena tunajongea kafeteria kupata staftahi. Kuna msururu mrefu wa wanafunzi. Awali, walemavu walipaswa kupanga foleni kama watu wengine. Baada ya jitihada za viongozi wa walemavu, sasa walemavu wanahudumiwa vizuri na wahudumu wa cafeteria.
Somo la sita: kwenye foleni na misururu inayochosha kama vile benki, mIgahawani, kwenye vyombo vya usafiri na hospitali, walemavu wapewe kipaumbele.
Ni usiku na giza linachukua sehemu yake. Mimi, Mzena na marafiki wengine tuko chumbani tukibadilishana mawazo. Ghafla anaingia Maingu Nyanjila, mwanamke aliyejitolea vya kutosha kwa ajili ya walemavu. Amekuja kumchukua Mzena akamsomee kitabu cha fasihi, ‘’Autobiography of Malcom X’’. Ni kitabu kikubwa lakini Mzena hana namna isipokuwa kumsikiliza Maingu akimsomea kurasa moja hadi nyingine. Hakuna vitabu katika maandishi maalumu ya nukta nundu(Braille). Vingekuwepo Mzena asingehitaji mtu wa kumsomea. Baadhi ya walimu wa chuo wanawapa walemavu notisi zao ambazo mzena anazisoma kwa vifaa vya kielektroniki vya kutunzia kumbukumbu au kompyuta yenye programu ya sauti. Darasani anapaswa kwenda na tepurekoda inayonasa mafundisho ya mwalimu. Kwa bahati mbaya, si kila kitu kinasemwa kwa sauti; baadhi ya mambo yanaandikwa ubaoni bila kuzungumzwa.

Somo la saba: Katika dunia ya leo ya kielektroniki, kuna vifaa vingi ambavyo vinaifanya elimu ya walemavu iwe rahisi na yenye tija. Jamii na wadau wote wa haki za walemavu wajitahidi kufadhili upatikanaji wa vifaa muhimu.
Kabla hawajaondoka chumbani kwenda maktaba au darasani kujisomea, ni desturi ya Maingu kuibua mjadala kuhusu mada ya kijamii. Ni vijana kutoka fani mbalimbali na kila mmoja analeta hoja yake. Mzena anatoa hoja kwa mtazamo wa kielimu na mimi naleta vifungu vya sheria. Maingu anaingilia na kutoa hoja ya kifasihi. Mara nyingi wanajua jinsi ya kunishinda. ’’Nyinyi wanasheria muna maneno mengi na hamtakwenda mbinguni kwa sababu hamtendi haki’’ Maingu angenitania ili kuidhoofisha hoja yangu.
Somo la nane: Walemavu washiriki kwenye mijadala ya kila siku ya makundirika. Marafiki wawape walemavu nafasi ya kutoa hoja zao na kuheshimu mitizamo yao. Walemavu wana tafakuri kama walivyo watu wengine.
Kuna mengi ya kuyazungumza kuhusu elimu shirikishi. Shule ya Msingi Nanjoka na Sekondari ya Frankweston nilikuwa swahibu wa mwanafunzi mwenzangu ambaye alikuwa mlemavu wakusikia. Ndanda nilisoma na walemavu wa macho. UDSM nimekutana na walemavu wa kila namna. Lakini, darasa maridhawa nimelipata nilipokata shauri kuishi na vicent Mzena, mlemavu wa macho. Natamani walemavu wote wangekuwa na moyo kama wa Mzena. Pia, nawausia vijana wenzangu na wanajamii kwa ujumla kuishi, kujenga urafiki na kuwakaribisha walemavu.
Lakini hali ikoje kwenye jamii? Utafiti uliofanywa na kituo cha taarifa kuhusu ulemavu( Information Centre on Disability-ICD) katika Manispaa ya Moshi, Mwanza na Morogoro kuhusu mchangamano baina ya walemavu na watu wasio na ulemavu, unaonyesha kuwa bado kuna changamoto katika kufanikisha mfumo shirikishi. Utafiti huo unaonyesha kwamba asilimia 57 ya watu kutokuwa na utayari na kukosa hulka ya upendo kwa walemavu wakati ni asilimia 47 tu ya watu ilionyesha kuwa na moyo wa kuwajali, kuwapenda na kuwakaribisha walemavu. Shime wanajamii tuibadili hali hii na kuishi kwa upendo na walemavu.
Inawezekana.Fanya tafakuri ya kina kisha chukua hatua.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba ya simu 0653619906. Barua pepe adoado75@hotmail.com

SOURCE :  http://www.facebook.com/ado.shaibu.3/posts/545137165537310

Monday, April 8, 2013

TANGAZO KWA WANAFUNZI WETU WA UALIMU WA UJASIRIAMALI

Tunapenda  kuwatangazia  wanafunzi  wetu  wote  wa  kozi  ya  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI  inayo  tolewa   chini  Mradi  Wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini  ( EUMIVI  -Project  )  kwamba  wanatakiwa  kuwa  wamekwisha  pokea  maswali  ya  mitihani  ya  nadharia  mpaka  sasa.  Kwa  wanafunzi  ambao  mpaka  sasa  bado  hawajapokea   maswali  ya  mtihani  wa   nadharia   tafadhali  tuandikieni  barua  pepe    ya  kutujulisha.
Imetolewa  na  Uongozi,
RafikiElimu   Foundation.