NAFASI ZA KAZI ( FOOD PRODUCTION ) RafikiElimu Education Consultancy ni Taasisi inayo jihusisha na usimamizi wa maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wanao soma katika shule za msingi na sekondari nchini Tanzania, pamoja na mafunzo ya ujasiriamali. Taasisi Kwa kushirikiana na shule mbalimbali za msingi na sekondari katika mikoa ya Dar Es Salaam na Mtwara inaratibu mradi wa “ MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA PIPI ZA VIJITI” almaarufu kama “ PIPI ZA KIHINDI”, kwa vijana waliomaliza kidato cha nne. Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea vijana hao , uwezo wa kujiajiri wenyewe kwa kutengeneza na kuuza pipi hizo kwenye shule za msingi na sekondari ambazo zinashirikiana na taasisi katika mradi huu. Kupitia mradi huu, taasisi inatangaza nafasi za kazi ya kufundisha namna ya kuandaa na kutayarisha pipi za vijiti ( Pipi za kihi...