RafikiElimu EDUCATION Consultancy ni Taasisi binafsi inayo jihusisha na USIMAMIZI wa MAENDELEO ya KITAALUMA kwa wanafunzi wanao soma katika shule za sekondari Tanzania.
Taasisi kwa makubaliano binafsi kati ya taasisi na mzazi/mlezi, inafanya kazi ya kufuatilia na kusimamia maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wanao soma katika shule za kutwa ( Day Scholars ) pamoja na wale wanao soma katika shule za bweni ( Boarding Scholars )
Taasisi ina toa huduma hii kwa wanafunzi wa sekondari waliopo ndani ya mkoa wa Dar Es Salaam, pamoja na wale waliopo nje ya mkoa wa Dar Es Salaam.
Vile vile, RafikiElimu EDUCATION Consultancy ina wasimamia pia wanafunzi wanao jiandaa na mitihani ya kidato cha nne, au sita kama watahiniwa binafsi ( Private Candindates ) , wanafunzi wanao jiandaa kurudia mitihani yao ya kidato cha nne au sita ( Reseaters), pamoja na wanafunzi wanao soma masomo ya kidato cha nne kwa programu ya miaka miwili au kidato cha tano na sita kwa programu ya mwaka mmoja.
Lengo kuu la taasisi ni kuhakikisha wanafunzi wote inao walea kitaaluma na kuwasimamia kitaaluma, wanafaulu kwa kiwango cha juu kabisa katika mitihani yao ya kidato cha nne na ile ya kidato cha sita.
Unaweza pia kuwasiliana nasi kupitia barua pepe yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.com
Mahindi ni miongoni mwa mazao ya chakula ambayo unga wake unatumika kutengeneza unga lishe. UNGA LISHE : Ni unga bora na unao hitajika sana katika kuborehs afya za watoto, wazee na wagonjwa. Ukiwa kama mjasiriamali mdogo, ni muhimu kujua namna ya kutengeneza unga lishe, kwani malighafi zinazo tumika katika utayarishaji wa unga huu zinapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu, hivyo basi hata kwa wewe mwenye mtaji mdogo, unaweza kufanya biashara hii bila ya kuhitajika kuwa na mtaji mkubwa jambo linalo chukuliwa...
Comments
Post a Comment