NAFASI ZA KAZI MTAFITI MSAIDIZI : NAFASI KUMI NA MBILI ( ATHARI ZA MIMBA ZA UTOTONI, ENEO LA MZINGATIO, LINDI & MTWARA) RafikiElimu Education Consultancy ni Taasisi binafsi inayo jihusisha na usimamizi wa maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wanao soma QT pamoja na wale wanao jiandaa kurudia mitihani ya sekondari ( Re-seaters). Taasisi ina andaa kitabu pamoja na documentary maalumu kuhusu ATHARI ZA MIMBA ZA UTOTONI katika wilaya mbalimbali zilizopo katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Kupitia project hii, Taasisi inatangaza nafasi kumi na mbili za kazi ya “ Mtafiti Msaidizi” atakae msaidia mwandishi mkuu wa kitabu hiki kupata taarifa muhimu zitakazo muwezesha kukamilisha zoezi la kuandika kitabu hiki. MAJUKUMU YA KAZI HII : ni pamoja na kuwatafuta wahanga wakuu wa tatizo la mimba za utotoni yani wasichana waliopata mimba utotoni na kuharibiwa ndoto zao za kuendelea na masomo yao kwa ajili ya kufanya mah...