Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2012

MAMA PINDA AWAAMBIA VIJANA UJASIRIAMALI NI AJIRA RASMI INAYOTAMBULIKA DUNIANI

Pichani Juu na Chini ni Mama Tunu Pinda akikagua baadhi ya mabanda na kujionea bidhaa mbalimbali katika maonyesho hayo. Mama Tunu Pinda akisoma kwa furaha kitini cha mafunzo ya Wajasiriamali baada ya kufungua Maonyesho ya Wanawake Wajasiriamali (MOWE) katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Hopolang Phororo na Noreen Toroka kutoka ILO. Mama  Pinda  akipokea  vitabu  toka  kwa  Noreen  Toroka ( Wa  Pili  kulia )  na  Hopolang  Phororo  wa  ILO. Mke wa Waziri Mkuu Mana Tunu Pinda akitoa hotuba ya kufungua Maonyesho ya Wanawake Wajasiriamali (MOWE) katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam ambapo amewahimiza wajasiriamali kujiunga katika ushirika ili iwe rahisi kusaidiwa kupata mikopo, kutafuta masoko, kupanga bei nzuri ya bidhaa zetu, kupata utaalam na teknolojia mpya. Kauli Mbiu ya ya Maonyesho hayo mwaka huu ni “Msichana Amka, Ujasiriamali ni Ajir...

Mradi Wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini Kuzinduliwa tarehe 01 NOVEMBA 2012.

Mradi  Wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini " EUMIVI -Project  " , unao  ratibiwa  na  Taasisi  Isiyokuwa  ya  kiserikali  ya  RafikiElimu  Foundation(  RAEFO  TANZANIA )   unatarajia  kuzinduliwa  rasmi  tarehe  01  NOVEMBA  2012 ,  kwenye  Ukumbi  wa  HEKO  HALL , uliopo  katika  eneo  la  SINZA - AFRIKA  SANA   jijini  Dar  Es  salaam. Akiteta  na  RAFIKIELIMU  BLOG ,  Msemaji  wa  Taasisi  ya  RAEFO  TANZANIA , Ndugu  Consolatha  THADEUS  amesema  ya  kuwa  ingawa  mradi  utazinduliwa, siku  ya  tarehe  01  NOVEMBA  2012, saa  tisa  kamili  Alasiri  lakini  mafunzo  yatakuwa   yakifanyika  asubuhi  na  m...

ORODHA YA MAJINA YA WALIO CHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA ELIMU YA UJASIRIAMALI JIJINI DAR ES SALAAM.

 Uongozi  wa  Taasisi  ya  RafikiElimu  FOUNDATION, unapenda  kuwafahamisha  wafuatao  kuwa wamechaguliwa  kujiunga  na  mafunzo  ya  ujasiriamali   yanayo  tolewa  bure  na  taasisi  chini  ya  Mradi  wake  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini.  "  EUMIVI - Project  ".  Uzinduzi  wa  mafunzo  haya na  mradi  kwa  ujumla    utafanyika  katika  ukumbi  wa  HEKO  HALL, uliopo  katika  eneo  la  SINZA - AFRIKA  SANA, karibu  na  kituo  cha  Daladala  cha  AFRIKA  SANA,  siku  ya  ALHAMISI  ya  tarehe  01  NOVEMBA  2012   saa  Tisa (  9  )   kamili  Alasiri hadi  Saa  kumi  na  mbili ( 12 )...

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOLEWA BURE

Taasisi   Isiyokuwa   ya   Kiserikali   ya   RafikiElimu   FOUNDATION   kupitia   Mradi   wake    ELIMU   YA   UJASIRIAMALI   MIJINI &   VIJIJINI   “ EUMIVI-Project “   inapenda   kuwatangazia   vijana   wote   wa   kitanzania   wenye   umri   wa   kati   ya   miaka   kumi   na   tano ( 15 )   hadi      Arobaini   na   Tano   (    45   )    nafasi   za   kushiriki   katika   mafunzo   ya   ujasiriamali. Mafunzo   yatakayo   tolewa   ni   pamoja   na : i.                      Utengenezaji   na   Uzalishaji   wa   Bidhaa   za   aina   mbalimbali   kama   vile   : ...