Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi zilizopo wilayani Tarime mkoa wa Mara wakifurahia msaada wa madawati zaidi ya 1,000 kutoka mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG). Wanafunzi wa shule za msingi za serikali za wilaya ya Tarime, mkoa wa Mara, wakikaa sakafuni kabla ya kupata msaada wa madawati zaidi ya elfu moja kutoka mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG). Msaada wa pikipiki tatu maarufu kama Bajaj ambazo mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) ulitoa kwa baadhi ya wananchi wa jamii zinazoishi karibu na mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara. TARIME Mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) umetoa msaada wa madawati zaidi ya 1,000 kwa shule za msingi zilizopo wilayani Tarime, mkoa wa Mara. Msaada huo utakaoen...