Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2012

ORODHA YA MAJINA YA WAJASIRIAMALI WA JIJINI DAR ES SALAAM WALIO JIANDIKISHA KATIKA MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI.

Yafuatayo  ni  majina   ya   vijana  wa  kitanzania  walio  jiandikisha  katika  awamu  ya  kwanza  ya   Mradi  wa  Elimu  ya Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini  "   EUMIVI   PROJECT . mbao  utaanza  rasmi  siku  ya  jumamosi  ya  tarehe  01  Septemba  2012   kuanzia  saa  nne  kamili  asubuhi  katika  Shule Ya  Msingi  Mlimani  iliyopo  katika  eneo  la  Chuo  Kikuu  Cha  Dar  Es  salaam.  Kwa  jijini  Dar  Es  salaam, mafunzo  yatachukua  siku  tatu, kuanzia  tarehe  01 Septemba  2012  hadi  tarehe 03 Septemba  2012. Baada  ya  hapo mradi  utaendelea  katika  miji  ya Arusha, Morogoro, Mwanza, Mbeya, Dodoma...

TAARIFA KUHUSU UZINDUZI WA MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI.

  Uongozi  wa   RafikiElimu  Foundation,   unapenda   kuwa  julisha    wajasiriamali  wote  walio  jiandikisha  katika   Mradi  Wa  Mafunzo  Ya  Ujasiriamali   Mijini & Vijijini , (  EUMIVI  PROJECT ) kwamba  mradi   utazinduliwa  rasmi  siku  ya   Jumamosi  ya  tarehe  01  Septemba   2012,   kuanzia  saa  nne  kamili  asubuhi   katika    eneo  la  Shule   Ya  Msingi  Mlimani  iliyopo  katika   eneo  la   Chuo  Kikuu  Cha  Dar  Es  salaam. Mambo  yatakayo  fanyika   katika  siku  ya  uzinduzi  ni  pamoja  na  kuutambulisha  rasmi  mradi  na  kuanza  kutoa  mafunzo...

Mitaala shule za msingi inawachanganya wanafunzi – Walimu

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Lwengera Darajani, wakiwa wakati wa mapumziko   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitopeni kutoka Wilaya ya Korogwe.   Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitopeni ya Mjini Korogwe, akizungumza na mwandishi wa habari hii   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Lwengera Darajani, wakiwa wakati wa mapumziko BAADHI ya walimu wa shule za msingi wilaya za Korogwe na Moshi wamelalamikia mabadiliko ya mara kwa mara ya mitaala kwa shule za msingi pamoja na idadi kubwa ya masomo kwa wanafunzi wa madarasa ya chini, kuwa yamekuwa yakiwachanganya wanafunzi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni walisema mabadiliko ya mara kwa mara kwa mitaala yanayofanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi bila maandalizi yamekuwa chanzo cha vikwazo cha kufanya vizuri kwa sekta hiyo. Akizungumza hivi karibuni na mwandishi wa habari hizi, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Gerezani, mjini Moshi, Khadija Mtui alisema mabadi...

BAJETI YA ELIMU TANZANIA, 2012/2013 ITAMALIZA AU KUPUNGUZA KERO HIZI?

Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Isensa ya wilayani Nkasi wakiwa darasa, darasa hili lina wanafunzi 211, mwalimu hana pa kukaa akifundisha hutoka nje kusubiri watoto wamalize kuandika. Shule ya msingi Selous iliyopo Namtumbo. Wanafunzi wa darasa la tano wakiwa darasani na mwalimu akifundisha. Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini. Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini. BAJETI ya elimu itasomwa bungeni siku ya Jumatatu, 13 Agosti 2012. Wakati bajeti ya Elimu inasubiriwa kwa hamu na wadau na hasa wapenda maendeleo ya Elimu, Baadhi ya maeneo nchini bado yanakabiliwa na changamoto kubwa sana hasa hali mbaya ya miundombinu, ukosefu wa vyumba vya madarasa na majengo ya shule ambayo yamesababisha baadhi ya shule kuweka madarasa ya nyasi kam...