RC Chalamila: Dar es Salaam kufuta shule zote za sekondari za kutwa ili kudhibiti nidhamu ya wanafunzi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wapo kwenye mchakato wa kufuta shule zote za sekondari za kutwa kwa ajili ya kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi wote wa sekondari. Chalamila ameyasema hayo katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Azania kwenye hafla ya kukabidhi magari kwa maafisa elimu wa sekondari kutoka wilaya nane, ambapo amesema, Mkoa wa Dar es Saalam una shule za sekondari 182 na za binafsi zipo nyingi zaidi ya 200. --- ILI kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wapo kwenye mchakato wa kufuta shule zote za Sekondari za kutwa. Chalamila ameyasema hayo leo Agosti 14, 2023 katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Azania kwenye hafla ya kukabidhi magari kwa maafisa elimu wa sekondari kutoka wilaya nane. Amesema, Mkoa wa Dar es Saalam una shule za sekondari 182 na za binafsi zipo nyingi zaidi ya 200. “Katika Mkoa tunapokea sh billion 1.3 fedha zinazohudumia wanafunzi kama ada na posho ya madar...