Baadhi ya wanafunzi wakihojiwa na mwandishi wa habari hii( hayupo pichani ) TAARIFA FUPI YA UCHUNGUZI JUU YA MATUKIO YA MIMBA KWA WANAFUNZI WILAYA YA HANDENI, MKOANI TANGA. UTANGULIZI Uchunguzi huu umefanyika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Uchunguzi umefanyika kuanzia Machi 19, 2013 katika Kata tatu za Wilaya ya Handeni, ambazo ni pamoja na Kata ya Chanika, Kata ya Vibaoni na Kata ya Kidereko. Uchunguzi huu wa kihabari ni mwendelezo wa utafiti uliofanyika Machi Mwaka jana (2012), kuangalia ukubwa wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia (GBV), katika vipengele vya Ubakaji, Watoto wa Kike Wanafunzi Kulazimishwa Kuolewa, Vitendo vya Ukeketaji, Vipigo kwa Wanawake pamoja na Vitendo vya Utelekezaji Watoto na Wanawake. Uchunguzi wa pili umefanyika kuangalia mrejesho wa matukio ya mimba na ndoa katika umri mdogo katika maeneo hayo, ikiwa ni mwaka mmoja tangu kufanyika kwa utafiti wa mwaka jana. MBINU ZA UCHUNGUZI...