Click image for larger version. 

Name: IMG_0078_0.JPG 
Views: 0 
Size: 80.2 KB 
ID: 212145

Ukifika nje ya geti la Kituo cha Masanga tangu mwezi huu wa 12 ulipoanza utakutana na huu ujumbe ''HAKATWI MTU HAPA'' hiki ni kituo cha kuzuia ukeketaji (TFGM) ambacho kinatoa mafunzo ya ukeketaji mbadala na tohara salama... kwa sasa kuna watoto zaidi ya 600 ambao wamekimbilia hapa ili wasikeketwe tangu msimu huu ulipoanza mwezi wa 12/2014...

Mwezi wa 12 ni mwezi wa kufanya tohara mkoani Mara ambapo watoto wengi huwa wamefunga shule na hivyo kupelekea watoto wa kike hukeketwa...


Click image for larger version. 

Name: IMG_0269_3-1.JPG 
Views: 0 
Size: 64.1 KB 
ID: 212146

Mabango haya yamebeba ujumbe tofautitofauti kwa lengo la kuifikishia jamii kilio chao kutokana na hii mila yao ya Ukeketaji...


Click image for larger version. 

Name: MSAADA TARIME(4).jpg 
Views: 0 
Size: 66.9 KB 
ID: 212138

Nimeona ni busara kuwaomba Umma tushirikiane kuwasaidia watoto hawa hasa kipindi hiki kigumu ambacho wamekimbia kukeketwa wakingojea msimu uishe mwezi huu wa 12 warudi makwao wakaendelee na shule... yaani hawana hata maji! kama ujuavyo maji ni muhimu sana kwa binadamu, na huwa wanategemea maji ya mvua!!! sasa mvua hazijanyesha hivi karibuni... pia hawana chakula, pedi, nguo, viatu, kama una maswali zaidi unaweza kumuuliza mkuu wa kituo hicho Sister Germana... Lakini chondechonde nakuomba tuwasaidie wako kwenye hali mbaya...

Habari hii nimeitoa www.wanawakelivetv.com